Friday, December 16, 2016
WAZIRI MKUU ACHARUKA...ASEMA NGO CHONGANISHI ZITAFUTWA
Do you like this story?
WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa miezi sita ya kujitathimini mashirika yasiyo ya kiserikali
(NGOs) yanayofanya kazi zake wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, kama yanafanya
kazi kwa misingi ya sheria na maadili.
Baadaye,
yatahakikiwa na kama yatabainika yanachochea migogoro, yatafutwa.
Pia,
Majaliwa amezicharukia NGOs nyingine zinazoitangaza vibaya Tanzania kimataifa
kwa kupiga picha za kudhalilisha watoto wakiwa wanatembea kwenye mawe huku
wamevaa kandambili kubwa, kuonesha nchi ni masikini. Ametaka NGOs hizo kuondoka
nchini, la sivyo serikali itazishughulikia.
“Hizi
NGOs zingine si muondoke, nendeni kwingine mkafanye kazi. Halafu nyie mnaotuma
picha za kudhalilisha watoto wakiwa wamevaa kandambili kubwa, kudai nchi za nje
eti Tanzania ni masikini, tutawashughulikia,” alisema Majaliwa alipozungumza na
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro jana.
Aidha
alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atakuja wilayani
hapo kukagua kazi walizozifanya, wanazozifanya na miradi wanaosaidia jamii.
Majaliwa
aliwaambia watumishi hao wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro pamoja na wadau
mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya serikali, yanayofanya
shughuli zake wilayani hapo, kuwa serikali haitaki mashirika chochezi wa
migogoro na itayafuta.
Alisema
serikali haitasita kuyafuta mashirika yanayofanya kazi wilayani humo, ambayo
yapo kwa nia ya uchochezi na kuacha kufanya kazi katika malengo yaliyokusudiwa.
Waziri
Mkuu alisema wilaya hiyo, ina mashirika yasiyo ya serikali 30 ambayo
yamesajiliwa, lakini yanayofanya kazi ni 19 tu.
Alisisitiza
kuwa haiwezekani serikali isajili mashirika hayo, lakini utendaji kazi wake uwe
hafifu.
Alisema
ukifuatilia, mashirika hayo utagundua kuwa yanapokea fedha nyingi, lakini
hakuna cha maana wanachokifanya kwa wananchi. Alisema serikali ina taarifa ya
NGOs hizo zinazopewa fedha na wafadhili.
“Najua
taarifa zenu mnapokea kiasi gani cha fedha na mnazifanyia nini, lakini namleta
Mkaguzi wa serikali ili akague mnatumiaje fedha zenu, nawapa miezi sita tu
halafu ukaguzi utaanza, maana kuna mashirika mengi lakini kazi mnazofanya
hazionekani,” alisema Majaliwa.
Alisema
baadhi ya mashirika, yana akaunti nchi jirani ya Kenya na mengine kama PWC
anapewa Sh bilioni 2.5 kwa mwaka na shirika la UCRT linapokea Sh bilioni 1.5
kwa mwaka, lakini hajui yanafanya nini.
“Nina
taarifa zenu mnapata hela nyingi, lakini mnahudumia vipi jamii hakuna, sasa
ngojeni ukaguzi ufanyike halafu nitachukua maamuzi maana kila siku Loliondo
kuna nini hapa mnasajiliwa halafu hakuna cha maana,” alisema.
“Kuna
nini Loliondo, kwani kila mara Loliondo nina taarifa za kila NGOs zinazofanya
kazi hapa, najua mnachokifanya, sasa nawaambia serikali haitawafumbia macho
kuona hiki ninachokifanya hapa na ikigundulika mnafanya kinyume na matakwa ya
usajili tutazifuta”.
Alisema
serikali itazifuta NGOs zote, ambazo zitabainika ni kiini cha migogoro
Loliondo. Alitoa hadhari kwa kampuni zinazofanya kazi zake bila usajili, kuwa
zikigundulika, zitachukuliwa hatua.
Aliwageukia
watumishi wa umma na kuwatahadharisha wale wanaotoa taarifa za migogoro ya
ndani kwa wahusika wa NGOs na kisha kuzituma nje ya nchi kwenye mitandao ya
kijamii na barua pepe.
Alisema
kuwa nao watashugulikiwa, kwa kuwa wanapaswa kuwa majibu ya migogoro na si
wasambazaji wa habari mbaya za nchi.
Alisisitiza
watekeleze kikamilifu kauli ya ‘Hapa Kazi Tu’ ; na si kutumia NGOs kwa ajili ya
kudai kuwasaidia wananchi, huku wakijua kuwa wananchi hawanufaiki na fedha hizo
wanazopewa na wafadhili Awali akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Wilaya
hiyo, Majaliwa alitoa tahadhari kwa madiwani kuacha kushirikiana na watu wa
Uhasibu wanaotoa hela kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema
baadhi ya madiwani, wanakwamisha miradi ya maendeleo kwa kula fedha kwa sababu
ya ukaribu walionao.
Akizungumzia
nidhamu ya fedha, Majaliwa alisisitiza kila mtumishi lazima afanye kazi kwa
bidii, ikiwemo kutoa huduma bila kuwabagua wananchi kwa itikadi zao za vyama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZIRI MKUU ACHARUKA...ASEMA NGO CHONGANISHI ZITAFUTWA”
Post a Comment