Monday, December 5, 2016

SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.



Bloggers wakifuatilia mada.



Serikali imetangaza rasmi kuitambua mitandao ya Kijamii (Bloggers) kuwa chombo cha habari nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk.Hassan Abbas Dar es Salaam leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN).

“Serikali sasa inaitambua rasmi mitandao ya kijamii kuwa ni chombo cha habari kama ilivyo vyombo vingine nchini hivyo nawaomba wakuu wa vitengo vya habari serikalini kushirikiana na wanamitandao hiyo katika kutoa taarifa mbalimbali” alisema Abbas.

Abbas alivitaka vyombo vya habari hasa magazeti pale wanapotumia picha kutoka mitandao ya kijamii kueleza chanzo cha picha hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo picha zao zinatumika bila ya kutaja chanzo.

Katika hatua nyingine Abbas alisema Bloggers haina tofauti na vyombo vingine hivyo ni vema wanapotoa habari zao kuzingatia sheria na weredi wa kazi vinginevyo sheria itawakumba kama ilivyo kwa magazeti na vyombo vingine.

Abass aliwataka wanamitandao hao kujiunga na TBN ili iwe rahisi kutatuliwa changamoto walizonazo kuliko kila mmoja kuwa kivyake.

Wanamitandao hao wakizungumzia changamoto waliyonayo walimwambia mkurugenzi huyo kuwa  wamekuwa wakibaguliwa na maofisa habari wa serikalini ikiwa pamoja na kunyimwa ‘Press Card’ jambo linalokwamisha utendaji wao wa kazi.

0 Responses to “SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)”

Post a Comment

More to Read