Wednesday, November 30, 2016

MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WAINGIA MTAANI KUKUSANYA MAPATO



Meya wa jiji la Mbeya David Mwasilindi


Halmashauri ya jiji la Mbeya imebuni njia mpya ya ukusanyaji wa mapato  ili kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa kiasi cha shilingi bilioni  11 katika  mwaka wa fedha wa  2016/17 .
Katika kufanikisha mpango huo halmashauri imewashirikisha madiwani na wataalmu wake katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani .

Moja ya njia hiyo halmshauri imeanza kuwatumia Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa katika ukusanyaji wa fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato .

Akielezea mkakati huo  Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Ndugu David Mwashilindi amesema katika kuhakikisha halmshauri inafikia lengo lake la ukusanyaji wa mapato imeamua kuongeza nguvu kazi kwa kuwaingiza madiwani na wenyeviti ambao wapo karibu na wananchi.

“ Kazi kubwa  wanayo ifanya madiwani na wenyeviti kwa kushirikiana na wataalam ni kuhakikisha wanavitambua vyanzo vyote vya mapato vinavyostahili kuingia katika mapato ya halmashauri  ikiwa na kubaini mianya iliyokuwa ikitumiwa na wahusika kukwepa kulipa kodi,”amesema Mwasilindi.

Amesema kuziendesha halmashauri hizi inategemea sana mapato ya ndani hivyo lazima kuweka jitahada za makusudi katika kufikia malengo husika .

Amesema katika kipindi cha nyuma halmashari hiyo hali ilikuwa katika hali mbaya kwani kwa mwezi walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 120 hadi 200 lakini mara baada ya kuanza kwa jitihada hizo imesaidia kupandisha mapato ambapo kwa sasa imefikia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa mwezi.

Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo sanjali na kukusanya mapato pia kuna sauala la utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuelewa namna ya kulipa  tozo zilizo wekwa kisheria.

Amesema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na mara baada ya hapo kutafanyika kwa tahimini ya pamoja ili kubaini changamoto zilizopo katika zoezi.

0 Responses to “ MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WAINGIA MTAANI KUKUSANYA MAPATO”

Post a Comment

More to Read