Tuesday, February 21, 2017
ALIYEFUKULIWA NA MAMA YAKE AZIKWA TENA
Do you like this story?
Hatimaye
serikali imeingilia kati sakata la Luth Segeleti(52)mkazi wa Shigamba Mbalizi
aliyefukua mwili wa mtoto Baraka Mfwango (22)aliyefariki februari 15 na kuzikwa
februari 16 na kufukuliwa na mama Mzazi kwa madai ya kumfufua februari 18 mwaka
huu ambapo serikali imeamua kuzika upya baada ya mama huyo kuridhia kufuatia
Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoa wa Mbeya Edwin Urio
kukutana naye katika kituo cha Polisi Mbalizi.
Akiongea kwa
kujiamini Luth Segeleti amesema kuwa mwanawe hajafa hivyo atafufuka endapo
atapelekwa hospitali ya Ifisi ili afufuke.Neema Mfwango dada wa marehemu
aliyefuatana na mjomba wake ameshukuru kwa uongozi kuchukua jukumu la kumzika
ndugu zangu yake.Kwa upande wake Mchungaji Edwin Urio amesema kuwa Luth si
muumini wa Kanisa hilo bali alifika kanisani hapo mwaka mmoja uliopita kwa
ajili ya maombi.
Naye
Mchungaji Lauden Mwafongo aliyeendesha Ibada ya mazishi amesema Luth Segeleti
si muumini wa Kanisa lake bali alimfahamu akija kwenye maombi kama watu wengine
wanavyokuja na kwamba alitoa huduma ya mazishi kama Mchungaji na si
muumini.Kikao kilichofikia muafaka kiliongozwa na Afisa Tarafa ya Usongwe Sadat
Mtwale,Diwani wa Nsalala Kissman Mwangomale maarufu kama KK , ndugu wanne wa
marehemu na mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi Debora Mrema ambapo Afisa
Tarafa ameonya juu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Baadhi ya
wananchi wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba Serikali kuwa makini na imani
potofu zinazoleta uvunjifu wa amani . Luth aliomba radhi kwa wakazi wa Shigamba
Mbalizi na viongozi wote kwani amedai imani ndiyo iliyomfikisha hapo na
hakushauriwa na mtu yeyote.Mazishi yamefanyika nje kidogo ya mji wa Mbalizi
tofauti na lile la awali kwa kuhudhuriwa na ndugu wanne wa Luth Segeleti pamoja
na viongozi wa Serikali huku mvua kubwa ikinyesha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ALIYEFUKULIWA NA MAMA YAKE AZIKWA TENA”
Post a Comment