Tuesday, February 21, 2017

VITA YA DAWA ZA KULEVYA YAHAMIA MAKANISANI



Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato mkoani Mara, George Ojwang’ amewaagiza wachungaji na wazee wa kanisa hilo kuwashughulikia waumini wao wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Aliyasema hayo katika sherehe za kumsimika mchungaji mpya wa Mtaa wa Mauwe ulioko Kitembe Rorya. Alisema kama kanisa litakuwa safi, Serikali haitakuwa na muda wa kushughulikia watu kama hao wanaosababisha kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa.
Katika tukio jingine, Mkoa wa Tabora umezindua kampeni ya kupambana na dawa za kulevya na wahusika wakionywa kutofanya mzaha katika vita hiyo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alisema tayari kamati zote za ulinzi na usalama za wilaya zimepewa maelekezo ya kufanya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema kati ya Februari 13 na 16 wamekamata dawa za kulevya mbalimbali zikiwamo cocaine, mirungi, bangi na mbegu zake.

0 Responses to “VITA YA DAWA ZA KULEVYA YAHAMIA MAKANISANI”

Post a Comment

More to Read