Saturday, February 18, 2017
AMEZA AINA SABA ZA DAWA ILI AJIUE KISA SHULE
Do you like this story?
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza
katika Shule ya Sekondari Milundikwa iliyoko katika Wilaya ya Nkasi
mkoani Rukwa mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa), mkazi wa
Kijiji cha Katani, amenusurika kufa baada ya kunywa aina saba za dawa
kwa lengo la kujiua akidaiwa hataki shule.
Akizungumza jana eneo la tukio, mama
mzazi wa mtoto huyo, Stella Hamis alisema juzi saa 2:00 asubuhi,
alimfokea mtoto wake huyo baada ya kumuona nyumbani badala ya kwenda
shule.
Stella alisema alimtaka mwanawe aende shule mara moja naye akaelekea shambani.
Hata hivyo, alisema baada ya muda mfupi,
mtoto wake huyo alijifungia ndani na kunywa dawa za hospitalini aina
saba tofauti zilizokuwapo na kuandaa kamba kwa ajili ya kujinyonga.
“Lakini kwa bahati mmoja wa wana familia,
aliingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta mtoto huyo akiwa hajiwezi
kutokana na dawa alizokunywa,” alisema.
Stella alisema taarifa zilisambaa kwa
jirani ambao walifika eneo la tukio la kumchukua mtoto huyo na kumpeleka
zahanati ya kijiji kwa matibabu.
Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Solana Kazikodi, alithitibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kazidosi alisema ofisi yake ilipata
taarifa mapema juu ya tukio hilo na ndiyo waliofanya kazi ya ziada
kuhakikisha mtoto huyo anakimbizwa haraka katika zahanati yao ya kijiji.
Alisema mtoto huyo alifaulu kuendelea na
masomo ya sekondari baada ya kufanya vizuri kwenye mtihani wa darasa la
saba katika Shule ya Msingi Katani.
Hata hivyo, alisema tangu aripoti katika shule hiyo, mahudhurio yake yamekuwa ni hafifu kutokana na kutopenda kusoma.
Mganga wa zahanati hiyo, Godfrey Manga,
alithibitisha kumpokea mwanafunzi huyo na kwamba alipatiwa matibabu na
hakuathiriwa kwa kiwango kikubwa na dawa hizo kwa kuwa walimuwahisha
zahanati kupata huduma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AMEZA AINA SABA ZA DAWA ILI AJIUE KISA SHULE”
Post a Comment