Saturday, February 18, 2017
AFUKUA MAITI YA MTOTO WAKE SIKU TATU BAADA YA MAZISHI MBEYA
Do you like this story?
Hili ndio Jeneza likiwa kwenye Gari ya Polisi kuelekea katika Hospitali ya Ifisi. |
Jeshi la Polisi wakiwa wamebeba Jeneza pamoja na watuhumiwa ambao wameusika katika kufukua Mwili huo |
Mara baada
ya Polisi kuondoka nyumbani kwa mtuhumiwa wananchi waliteketeza kwa moto nyumba
ya Luth.(Picha na Ezekiel Kamanga Mbeya)
|
Wananchi wakishuhudia tukio |
Luth
Segeleti (52)mkazi wa shigamba Mbalizi Wilaya ya Mbeya anashikiliwa na Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya baada ya kufukua kaburi la mtoto wake kisha mwili kurudi
nao nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya maombi ili afufuke.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Dhahiri
Kidavashari amesema marehemu Baraka Mwafongo (22)alifariki February 15 na
mazishi kufanyika Februari 16 mwaka huu, lakini mama Mzazi Luth Segeleti
anayeabudu Kanisa la Ufufuo na Uzima alidai mwanawe atafufuka siku ya tatu.
Kidavashari
amesema kuwa Luth alianza zoezi la ufukuaji saa sita usiku na kumaliza zoezi
hilo mapema alfajiri kwa kushirikiana na vijana wawili akiwemo mwanawe.
Aidha
aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda nao nyumbani kwake kisha kuogesha na
kuupaka mafuta tayari kwa maombi.
Hata hivyo baadhi ya majirani walimtilia shaka
Luth baada ya kumkuta na jembe akiwa ametoka makaburini na walipomuuliza
alikiri kufukua na kudai kuwa mwanawe hajafa hivyo atafufuka baada ya
maombi.Wananchi walitoa taarifa Polisi ambao walifika eneo la tukio na kumhoji
Luth ambapo alikiri kufukua kaburi la mtoto wake hivyo Polisi walichukua jeneza
tupu na mwili kuupeleka hospitali teule ya Ifisi kwa uchunguzi zaidi.
Mara baada
ya Polisi kuondoka nyumbani kwa mtuhumiwa wananchi waliteketeza kwa moto nyumba
ya Luth ambapo Jeshi la Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbalizi wakiongoza na mkuu wa
Polisi Wilaya hiyo Debora Mrema kufanya kazi ya ziara kuzima moto huo.
Baadhi ya
watu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo la uchomaji moto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AFUKUA MAITI YA MTOTO WAKE SIKU TATU BAADA YA MAZISHI MBEYA ”
Post a Comment