Saturday, February 18, 2017

MBUNGE WA SHINYANGA 'AMJARIBU' MAGUFULI


Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele ameitaka serikali kutumbua kuwa wananchi wanakabiliwa na njaa, na hawezi kutumbuliwa kwa kusema ukweli kwakuwa amechaguliwa na wananchi.
Alisema hayo wakati wa ziara yake jimboni humo ambapo kila kata aliyopita alikumbana na vilio vya wananchi wakilia njaa, huku watendaji wa serikali wakilifumbia macho suala hilo kwa kuhofia kutumbuliwa.
Masele alisema hawezi kuvumilia suala la njaa wakati wapiga kura wake wanashindia uji na wengine kukosa kabisa chakula, hivyo ni bora serikali ikapanga utaratibu wa kugawa chakula cha msaada hata kama ni kuuza kwa bei nafuu.
“Wananchi wangu wanalala njaa, hivyo mimi siwezi kuogopa kusema ukweli, na Rais anataka watu wafanye kazi lakini hawawezi kufanya hizo kazi sababu wana njaa.
Kauli ya Mbunge huyo inaonekana kumjaribu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa tarehe 11 Januari, 2017 alipokuwa katika ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza  watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi.
Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la njaa.
” Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe kuuza chakula nje ya nchi kwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa”

0 Responses to “MBUNGE WA SHINYANGA 'AMJARIBU' MAGUFULI”

Post a Comment

More to Read