Friday, February 24, 2017

ASHITAKIWA KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO QURAN


WhatsApp Image 2017-02-24 at 11.43.46 AM
Mwanaume mmoja raia wa Denmark aliyechoma Quran ameshtakiwa kwa tuhuma za kukufuru ikiwa ni shtaka la kwanza ya aina hiyo nchini humo kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.
Mshtakiwa huyo — jina lake kamili halijawekwa wazi kwakuwa Sheria za nchini Denmark haziruhusu kutaja jina la mtuhumiwa mpaka pale atakapopatikana na hatia — mwaka jana alifunguliwa mashtaka kwa kutoa kauli za chuki, lakini shtaka hilo sasa limebadilishwa na kuwa la kufuru dhidi ya dini nyengine. Uamuzi huu ulitangazwa Jumatano na waendesha mashtaka jijini Viborg, Denmark.
Mwanaume huyo mwenye miaka 42 alichoma kitabu kitukufu katika Uislam nyuma ya nyumba yake mwezi Disemba mwaka 2015, kisha akaweka video ya tukio hilo kwenye kundi alilopo katika mtandao wa kijamii wa Facebook – akiandika ujumbe uliosomeka: “Mjali jirani yako: “kitabu hiki kinanuka wakati kinaungua,” alisema Jan Reckendorff, muendesha mashtaka mkuu katika kesi dhidi ya mwanaume huyo.
Hii ni mara ya nne kwa mtu yeyote yule kuwahi kufikishwa Mahakamani kwa kosa la kukufuru dini katika historia ya Denmark toka kuanzishwa kwa utekelezaji wa sheria hiyo.
Waendesha Mashtaka wanasema kuwa, kuchoma vitabu vitukufu vya dini kama Quran na Biblia ni kukiuka sheria za nchi hiyo zinazohusiana na kukejeli dini au kudhihaki dini mbele ya kadamnasi.
Kushawahi kupatikana kwa hatia mbili tu tangu kuanza kutekelezwa kwa sheria hii – mwaka 1938 na mwaka 1946. Shtaka jengine lilifikishwa Mahakamani mwaka 1971, lakini mtuhumiwa hakupatikana na hatia.
Kifungo cha juu cha kukaa gerezani kwa kosa hili la kudhihaki dini nchini Denmark ni miezi minne, lakini Reckendorff anasema kuwa kama akipatikana na hatia, atatozwa faini tu.

0 Responses to “ASHITAKIWA KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO QURAN”

Post a Comment

More to Read