Friday, February 24, 2017
SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA DESTURI YA KUNUNUA KAZI ZA WASANII
Do you like this story?
Serikali
imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii, kwakuwa ndiyo
njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.
Wito
huo umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na
Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tovuti
a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za muziki za wasanii.
Alisema
mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu ya kupambana na wezi wa kazi
za wasanii, kwakuwa video za muziki zitakuwa zikipatikana kwenye mtandao huo
peke yake kwa kipindi maalum na hivyo kuingiza pesa zinazoenda kwa msanii,
serikali na watayarishaji moja kwa moja.
Pia
alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili zaidi,
itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya lugha elfu sita
duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje, wizara yake itawaunganisha
na Watanzania waliopo nje ya nchi.
Prof
Ole Gabriel amewataka wasanii wao wenyewe kuunga mkono mpango huo sababu ndio
njia pekee ya kuufanya ufanikiwe.
“Mpango
huu utafanikiwa kama ninyi mkiwa sehemu ya mpango huu, kama ninyi wenyewe tena
mkianza kuwa na kona kona na kuupiga vita, basi mpango huu utaonekana feki na
utashindikana,” alisema.
Hadi
sasa kuna video mbili mpya zilizowekwa kwenye Afro Premiere ambazo ni Go Low ya
G-Nako na Jux pamoja na K wa Roma na Baghdad. Mashabiki wanaweza kununua nyimbo
hizo kwa shilingi 300 tu kwa kutumia simu zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA DESTURI YA KUNUNUA KAZI ZA WASANII”
Post a Comment