Friday, February 24, 2017
MGOSI: TUMEJIANDAA KUSHINDA
Do you like this story?
WAKATI
wakitarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam leo jioni tayari kuwavaa mahasimu
wao, Meneja wa timu ya Simba, Mussa Hassan 'Mgosi' amesema kesho
atawathibitishia mashabiki na wanachama wa timu hiyo yeye ni meneja na kikosi
chake wako makini.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mgosi, alisema kuwa kikosi chake kimefanya maandalizi yote sahihi yanayotakiwa na sasa wanasubiri kazi moja ya kuonyesha vitendo.
Mgosi alitamba kuwa kikosi chake kiko imara msimu huu na hiyo ilijidhihirisha katika mechi ya mzunguko wa kwanza licha ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 60, Yanga ilishindwa kuondoka na pointi tatu.
"Tuko tayari kwa mchezo wa Jumamosi, tumejiandaa kushinda kwa sababu lengo letu ni kutwaa ubingwa, ukitaka kuamini hawatuwezi, walishindwa kutufunga tukiwa pungufu katika mechi ya kwanza," alisema Mgosi.
Meneja huyo aliongeza kuwa watasikia furaha zaidi ya kutwaa ubingwa msimu huu kwa kutangaza kupitia mechi hiyo ya kesho ambayo mbali na kuwafunga watani zao, pia watakuwa wamewavua ubingwa.
Kuhusu wachezaji majeruhi, Mgosi alisema kuwa ripoti kamili itatolewa na daktari wa timu hiyo baada ya kumaliza mazoezi ya leo asubuhi.
Simba ndiyo vinara katika ligi hiyo wakiwa na pointi 51 wakifuatiwa na Yanga yenye pointi 49, lakini wana pungufu ya mechi moja.
Wakati huo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Laudit Mavugo, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo wa Januari.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MGOSI: TUMEJIANDAA KUSHINDA”
Post a Comment