Friday, February 17, 2017
MANATI KUBWA YA KURUSHA DAWA ZA KULEVYA YAGUNDULIWA
Do you like this story?
Manati hiyo inaonekana kuundwa mahsusi kwa ajili ya kurusha dawa za kulevya hadi Marekani.
Marekani imekuwa ikikabiliana sana na walanguzi wa mihadarati kutoka Mexico pamoja na wahamiaji.
Rais Donald Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu sana kuzuia hilo.
Manati hiyo kubwa iligunduliwa na maafisa kusini mashariki mwa Tucson, Arizona, wiki iliyopita.
Wanasema waliwaona wanaume kadha wakitawanyika na kutoroka walipogundua kwamba maafisa hao walikuwa wanafika.
Maafisa hao walipokagua eneo hilo, waligundua vifurushi viwili vya bangi, vilivyokuwa na bangi ya jumla ya kilo 21.
Vifurushi hivyo vilikuwa bado havijarushwa.
Manati hiyo ambayo ilikuwa imejengwa upande wa Mexico wa ua ilibomolewa.
Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.
Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.
Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu lakini walanguzi wamekuwa wakitumia ubunifu katika kutumia njia za kufikisha madawa Marekani.
Miongoni
mwa njia hizi ni kutumia ndege ndogo zisizo na marubani na wakati
mwingine kuchimba njia za chini kwa chini zinazofika hadi Marekani.
Mwezi
Machi, maafisa waligundua njia ya chini kwa chini ya umbali wa mita 380
ambayo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja Mexico hadi kwenye jumba
moja California.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MANATI KUBWA YA KURUSHA DAWA ZA KULEVYA YAGUNDULIWA ”
Post a Comment