Thursday, February 16, 2017
Tundu Lissu: Serikali haiwezi kuifuta TLS
Do you like this story?
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe jana alisema kuwa atakifuta
Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society (TLS)) kwa
madai kuwa kimesahau misingi yake na kuanza kufanya kazi kama chama cha
siasa.
Waziri
Mwakyembe alisema kuwa, kama wanataka kufanykazi kama chama cha siasa,
basi yeye ataongea na msajili wa vyama vya siasa nchini ili cha hicho
kipya kisajiliwe.
Kufuatia
kauli hiyo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki na
mgombea Urais wa TLS, Tundu Lissu ameandika waraka huu kwenda kwa
wanasheria wenzake.
Mawakili
wenzangu. Mimi binafsi sijashangazwa na kauli ya Dkt. Mwakyembe kwamba
ataifuta TLS kama itajiingiza katika harakati za kisiasa. Hii sio mara
ya kwanza kwa viongozi wa serikali ya Tanzania kutoa vitisho vya kuifuta
TLS.
Waziri
Mkuu hayati Edward Sokoine aliwahi kutishia hivyo katika kilele cha
vita dhidi ya wahujumu uchumi miaka ya mwanzo ya ’80. Na hata kabla ya
hapo katika miaka ya ’60 na ’70 watangulizi wa Sokoine walijaribu
kufanya hivyo hivyo. In fact, kuanzishwa kwa Tanzania Legal Corporation
kipindi hicho kulikuwa driven in part na jitihada za kuondoa the private
bar.
Vitisho
dhidi ya TLS vilirudi miaka ya ’90 wakati wa Lyatonga Mrema. Kitu
kimoja kiko common katika vitisho hivyo vyote. Vitisho hivi vimetolewa
kila wakati TLS na private bar wanapo-assert their independence na
wanapoanza kutetea utawala wa sheria na kupinga state lawlessness and
impunity of the rulers.
Mawakili
wakiwa kimya na TLS ikiwa mfukoni mwa serikali na wasipohoji matumizi
mabaya ya madaraka basi wanakuwa darlings wa serikali.
Kuna
kitu kingine ambacho ni common katika vitisho hivi. Havijawahi
kufanikiwa na havitafanikiwa. Sheikh Abeid Amani Karume alipiga marufuku
private legal practice mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya ’64.
Tanzania ya leo sio Zanzibar ya miaka ya ’60 na ’70, hatutakubali
udikteta wa aina ya Karume au wa aina nyingine yoyote kwenye Tanzania ya
leo.
Inaelekea
Dkt. Mwakyembe hafahamu au anajisahaulisha jinsi ambavyo TLS na
mawakili binafsi walivyo embedded kwenye mfumo wetu wa kikatiba na
kisheria. Simply put, ukifuta TLS maana yake ni kwamba hakuna wakili
binafsi hata mmoja nchi nzima. Mfumo mzima wa kimahakama unategemea
uwepo wa mawakili na kwa hiyo uwepo wa TLS. Mahakama karibu zote
zitashindwa kufanya kazi kusipokuwa na mawakili binafsi. The same
applies to various tribunals and other judicial and quasi judicial
bodies.
Aidha,
kuna taasisi nyingi zilizoundwa na Katiba yetu kama vile Judicial
Service Commission na Law Reform Commission ambazo zinakuwa properly
constituted kukiwa na uwakilishi wa TLS. Kuna taasisi nyingine nyingi
ambazo zimeanzishwa na sheria za kawaida ambazo composition yake
inakamilika kukiwa na representation ya TLS. Hiyo legal, constitutional
and political upheaval itakayotokana na kufutwa kwa TLS will be
unprecedented and unimaginable kwa mtu mwenye akili timamu.
Dkt.
Mwakyembe ana akili timamu. He must be joking. Hawezi kufuta TLS.
Anachotaka kufanya ni kuwatisha mawakili ili wachague watu wale wale wa
miaka yote kuongoza TLS. Anatutisha ili tuendelee na status quo katika
uongozi wa TLS. Hataki tufanye mabadiliko yanayohitajika ili TLS yetu
isichukue nafasi yake stahiki katika kuamua mustakbala wa nchi yetu na
wa taaluma yetu.
Nawataka
viongozi na wanachama wa TLS wamkemee Dkt. Mwakyembe in the strongest
possible terms. Nawataka wagombea wenzangu wa nafasi mbali mbali za
uongozi katika TLS wajitokeze hadharani na kulaani kauli ya Dkt.
Mwakyembe in no uncertain terms. Wakinyamaza tutawajua wako upande wa
nani: status quo au mabadiliko. And I’ll ask you all to vote
accordingly.
Tundu Lissu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Tundu Lissu: Serikali haiwezi kuifuta TLS”
Post a Comment