Thursday, February 16, 2017
ANDY PUZDER,ALIYETEULIWA NA TRUMP KUWA WAZIRI AJITOA
Do you like this story?
Andrew
Puzder, aliyekuwa ameteuliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kuwa waziri wa
masuala ya wafanyakazi, amejiondoa muda mfupi kabla yake kuhojiwa na wabunge.
Puzder
alipoteza uungwaji mkono wa maseneta kadha wa chama cha Republican baada yake
kukiri kwamba alimwajiri mhamiaji aliyeingia Marekani kinyume cha sheria kuwa
mjakazi.
Bilionea
huyo pia amekosolewa kwa matamshi yake kuhusu wanawake na wafanyakazi katika
migahawa yake.
Yeye
sasa anakuwa mtu wa kwanza miongoni mwa waliopendekezwa na Trump kuwa waziri
kukosa kuidhinishwa.
Talaka
yake na mkewe mwaka 1980, ambayo ilikumbwa na mvutano mkubwa, pia imemwathiri.
Majuzi,
ilibainika kwamba mke wake wa zamani, Lisa Fierstein, alishiriki kama
mwathiriwa wa udhalilishaji kwenye ndoa katika kipindi cha Oprah Winfrey mwaka
1990 ambacho kilifahamika kwa jina High Class Battered Women (Wanawake wa
tabaka la juu wanaopigwa na waume zao).
Walitalikiana
mwaka 1987, lakini baadaye aliondoa tuhuma . za udhalilishaji dhidi ya Puzder
wakati wa makubaliano kuhusu nani angewatunza watoto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ANDY PUZDER,ALIYETEULIWA NA TRUMP KUWA WAZIRI AJITOA”
Post a Comment