Thursday, February 16, 2017
MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI MBEYA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUJIUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA
Do you like this story?
JESHI la polisi Mkoani Mbeya, linamshikilia mfanyabiashara maarufu
Jijini Mbeya, Steven Samweli (Maranatha), kwa tuhuma za kujihusisha na biashara
za dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema kuwa
Maranatha, alikamatwa juzi, kwenye moja ya duka lake la biashara za dawa baridi
kwa matumizi ya binadamu.
Alisema, baada ya polisi kupata taarifa za kuhusishwa kwa mfanyabiashara
huyo na mtandao wa dawa za kulevya, liliweka mtego na hatimaye kufanikiwa
kumtia nguvuni na sasa anahojiwa.
Aidha, kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, kunafikisha idadi ya watu nane
wanao tuhumiwa kujihusisha na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za
kulevya Mkoa wa Mbeya, huku watumiaji wanaoshikiliwa wakiwa ni 23.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI MBEYA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUJIUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA”
Post a Comment