Monday, February 13, 2017
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEWATAJA WATUHUMIWA ZAIDI 25 WA DAWA ZA KULEVYA
Do you like this story?
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 13.02.2017.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya
limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo
mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na
wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na
wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio
makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu
wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa
wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio
yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-
KUKAMATA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA
NA BIASHARA YA UUZAJI/USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.
Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako
katika maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha
na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji na
watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha ba
usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1. SHABAN RAMADHAN [40]
Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35]
Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA [60]
Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN
[22] Mkazi wa Airport - Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde.
Watuhumiwa
wote wapo mahabusu na mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa
watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.
KUKAMATA WAUZAJI/WASAMBAZAJI WA DAWA
ZA KULEVYA.
Aidha
kufuatia misako iliyofanyika kuanzia
tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo mbalimbali Mkoani
Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio mawili tofauti wakiwa na
dawa za kulevya.
Katika
msako wa kwanza uliofanyika maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na Mkazi wa Ilemi
alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa
za kulevya aina ya Heroine.
Pia
katika msako uliofanyika maeneo ya Mbalizi, ANITHA ABEL [21] Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika shule ya
Sekondari Sanani iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na Mkazi wa Mbalizi
alikamatwa akiwa na kete 15 za dawa
za kulevya aina ya Heroine akiwa nyumbani
kwao.
Mtuhumiwa
anaishi na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la MARTHA MWALINDU ambaye alikimbia baada ya kuwaona askari na
inasadikika ndiye muuzaji/msambazaji mkubwa wa dawa hizo za kulevya na huwa
anamtumia mtoto wake kuuza na kusambaza. Msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa
zinaendelea.
Watuhumiwa
hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya Upelelezi kukamilika.
KUKAMATA WATUMIAJI WA DAWA ZA
KULEVYA [MATEJA].
Aidha
katika misako mbalimbali iliyofanyika walikamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na
utumiaji wa dawa za kulevya maarufu kama Mateja
ambao ni:-
•
AYUBU
ABDALLAH [42] Mkazi wa Ilomba jijini Mbeya
•
EMANUEL
SIMBEI [43] Mkazi wa Sokomatola
•
IMAN ABBAS
[33] Mkazi wa Majengo
•
SHABAN
SHAIBU [19] Mkazi wa Nonde
•
KENY SANGA Mkazi wa
Sokomatola
•
PASCHAL
PIUS [28] Mkazi wa Itiji
•
PILIM
KAYANGE [20] Mkazi wa Uhindini
•
ELISHA
MWAIHABI [19] Mkazi wa Nonde
Wengine
ni:-
•
DANIEL
KANJANJA [43] Mkazi wa Uhindini
•
MUSSA
KIPESA [37] Mkazi wa Iwambi
•
CHARLES
GERVAS [28] Mkazi wa Nonde
•
KIMANZI
KILONZA [44] Mama John
•
SHABAN
SHAIBU [26] Mkazi wa Nonde
•
EMANUEL
LUCAS [18] Mkazi wa Ilomba
•
RICHARD
GONDWE [40] Mkazi wa Ivumwe
•
HENRY LEMA
[35] Mkazi wa Mama John
•
RAMADHAN
ABBAS [18] Mkazi wa Sae
•
EDWARD
MWASEKA [30] Mkazi wa Majengo
•
LUSEKELO
KIDION [26] Mkazi wa Mwakibete
•
ALINANUSWE
STIVEN [26] Mkazi wa Ilolo
•
JUSTIN
WISTON [23] Mkazi wa Mafiati
•
MICHAEL
KASHILILIKA [20] Mkazi wa Manga
•
KANI
ASANGALWISYE [28] Mkazi wa Ituha.
Watuhumiwa
wapo mahabusu wanaendelea kuhojiwa ili kupata mtandao halisi wa wauzaji na
wasambazaji wa dawa za kulevya.
KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA
[BHANGI].
Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako
dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Katika
misako hiyo iliyofanyika maeneo ya Mabatini na Ilomba jijini Mbeya, watuhumiwa
wanne walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi misokoto mitatu
yenye uzito wa gram 15.
Watuhumiwa
waliokamatwa ni 1. GEOFREY ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini 2.
ZUBER MWAMBENYA [24] 3. GWAKISA ANYOSISYE
[20] wote wakazi wa Mama John na 4. PHILIBERT MOSES [35] Mkazi wa Nonde.
KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.
Mnamo
tarehe 11.02.2017 majira ya kuanzia saa 17:00 hadi saa 17:45 jioni
msako ulifanyika maeneo ya Soweto Mtaa wa Mkombozi, Kata ya Ruanda na maeneo ya
Nonde, Kata ya Nonde, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa
kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na miche ya Bhangi 18 na mbegu zake.
Watuhumiwa
hao ni 1. DENIS DAVID [30] Mkazi wa Soweto ambaye alikamatwa
akiwa dukani kwake na 2. STIVIN VENANCE
[18] Mkazi wa Nonde. Upelelezi
unaendelea.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na mahojiano na watuhumiwa ili kuweza
kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha nao katika biashara ya dawa za kulevya.
KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO]
Mnamo
tarehe 10.02.2017 majira ya saa 21:00 usiku katika msako
uliofanyika huko maeneo ya Mafiati, Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na
Mkoa wa Mbeya watuhumiwa wawili walikamatwa wakiwa na Pombe Moshi ujazo wa lita 10.
Watuhumiwa
hao ni 1. FRANCIS NDEZI [32] Mkazi wa Forest na 2. JAMES KAJANJA [38] Mkazi wa Forest ya Zamani. Upelelezi unaendelea.
KUKAMATA WATUHUMIWA WANAJIHUSISHA NA
MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA NA KUTEKA MAGARI.
Mnamo tarehe 12.02.2017 kuanzia majira ya saa 20:00 hadi saa 23:45 Usiku, Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko katika vijjiji vya Mabadaga na
Mpakani vilivyopo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya jirani na barabara kuu ya
Mbeya kwenda Njombe. Msako huo ulilenga kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na
matukio ya unyang’anyi wa kutumia na silaha na utekaji magari wakati wa usiku.
Katika
msako huo jumla ya watuhumiwa 11 wamekamatwa
ambao ni 1. EMANUEL MANGA [30] Mkazi wa Njombe 2. ZAWADI MAKOGA [33] Mkazi wa Makambako 3.
ISSA ABIBU [45] Mkazi wa Mbeya 4.
FRICK MCHAMI [26] Mkazi wa Machimbo 5.
MPAJI KAPUNGU [38] Mkazi wa
Lugelele na 6. RICH KIHOMBO [25] Mkazi wa Ubaruku.
Wengine
waliokamatwa ni 7. MUSSA MTWEVE [27]
Mkazi wa Machimbo – Mbarali 8. WILBERT
MAGAINA [36] Mkazi wa Mlomboji 9. IBRAHIMU TWEVE [35] Mkazi wa Mlomboji – Mbarali 10. JOHN MBAFO [48]
Mkazi wa Machimbo na 11. ZABRON MWILONGO
[20].
Aidha
katika msako huo Pikipiki 4
zilikamatwa baada ya watuhumiwa kuwaona Polisi na kuzitelekeza na kukimbia.
Pikipiki hizo ni yenye namba 1. MC 254 BHK aina ya Kinglion 2. MC
264 AZZ aina ya Kinglion 3. MC 521 BYC aina ya Sanlg na 4. MC 565 BGE aina ya Kinglion.
Upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na
matukio hayo.
KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU.
Mnamo
tarehe 13.02.2017 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Eneo na Kata ya
Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, wahamiaji haramu watatu wote
raia na wakazi wa nchini Ethiopia walikamatwa kwa kosa la kuingia nchini bila
kibali.
Wahamiaji
hao ni 1. AGAFA SHAMENO [22] 2. BEKELE
SEDESO [29] na 3. SESEBE
SHIFUHA [24]. Upelelezi unaendelea.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A.
KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa
kuwafichua watu na mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Aidha Kamanda
KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi
kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani
inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya
mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Imesainiwa
na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEWATAJA WATUHUMIWA ZAIDI 25 WA DAWA ZA KULEVYA”
Post a Comment