Monday, February 13, 2017
MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOSI MAKALLA ALIAGIZA JIJI LA MBEYA KUKARABATI BARABARA ZA KATA YA RUANDA NA KULIWEKA JIJI LA MBEYA SAFI
Do you like this story?
Mwonekano wa Barabara ambayo wananchi wameilalamikia kuwa imesahaulika kwa muda mrefu. |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipewa maelezo na Mwananchi wa eneo la Ruanda Maarufu kwa Chaula(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya) |
Mkuu wa Mkoa
amemwagiza Mhandisi wa Barabara Jiji la Mbeya kuhakikisha wanaanza kazi ya
kutengeneza barabara hiyo mara moja ili wananchi waondokane na kero hiyo.
Makalla
alitoa agizo hilo baada ya kuelezwa kuwa katika ratiba za Jiji barabara hiyo
inaanza kutengenezwa keshokutwa.
Mbunge wa
jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kwa kazi nzuri ya kushungulikia kero za wananchi. (Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya) |
Mbunge wa
Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aambaye pia alikuwepo kwenye ziara
hiyo, alisema wakati yuko bungeni alipokea simu nyingi za wananchi wa eneo hilo
wakilalamikia barabara hiyo na kwamba baada ya kusikia Mkuu wa Mkoa anaenda
aliona ni vema nay eye ashiriki.
Alimshukuru
Mkuu wa Mkoa kwa kushughulikia kero za wananchi kwa kwenda katika maeneo yenye
matatizo ili nay eye ajionee na kuwasikiliza kisha kufanya maamuzi.
Sugu alisema
kutokana na kero hiyo ni vema Jiji likaiweka kwenye mambo yake ya dharura ili
kuwasaidia wananchi hao hasa kipindi hiki cha mvua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOSI MAKALLA ALIAGIZA JIJI LA MBEYA KUKARABATI BARABARA ZA KATA YA RUANDA NA KULIWEKA JIJI LA MBEYA SAFI”
Post a Comment