Tuesday, February 28, 2017

MENGINE YAIBUKA JUU YA ALIYEJIKATA UUME WAKE SINGIDA


Jeshi la Polisi mkoani Singida, linamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kujaribu kujiua baada ya kukata kwa panga  uume wake hadi kuutenganisha kabisa na mwili, kwa madai ya kuchoka kuhangaika na ugumu wa maisha unaomkabili.
Mwanaume  huyo Ntandu Mahumbi  mkulima na mkazi wa Kijiji cha Maghojoa wilaya ya Singida, anadaiwa kutenda kosa hilo juzi saa tano asubuhi, muda mfupi baada ya kurejea nyumbani akitoka kulima shambani.
Alisema mzee Mahumbi amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa chini ya ulinzi wa askari polisi,na pindi uchunguzi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya kutaka kujiawa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magilingimba alisema tukio hilo la kusikitisha, limetokea Februari 23 mwaka huu huko katika kijiji cha Maghojoa.
Katika tukio la pili, Magiligimba alisema mkulima wa kijiji cha Mwanyonye kata ya Ikhanoda wilaya ya Singida, Salome Mwanga (55) amefariki dunia baada ya kupigwa kichwani kwa jiwe na mtoto wake Ally Ramadhani (30).
Alisema kuwa kifo  hicho kimechangiwa na mgogoro wa kugombea shamba.
Kamanda huyo alisema tukio hilo limetokea Februari, 21 mwaka huu saa nne asubuhi huko katika kijiji cha Mwanyonyi kata ya Ikhanoda.
Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa Ally alikuwa analima katika shamba lililopo jirani na nyumbani kwao ambalo mama yake pia hulilima.
“Salome alimwendea Ally na kumtaka asiendelee kulima katika shamba hilo,na Ally aligoma na kumwangiza mama yake aondoke haraka hapo shambani.Salome hakuondoka kitendo kilichosababisha Ally aokote jiwe na kumpiga kichwani na kumsababishia kupata jereha na maumivu makali,” alisema Magiligimba.
Alisema Salome aliweza kukimbizwa katika kituo cha afya cha Ilongero kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Hata hivyo ilipofika saa mbili usiku,alifariki dunia.
Alisema wanamshikilia Ally na pindi uchunguzi utakapokamilika,atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji.

0 Responses to “MENGINE YAIBUKA JUU YA ALIYEJIKATA UUME WAKE SINGIDA”

Post a Comment

More to Read