Tuesday, February 28, 2017

ZAIDI YA WANANCHI MILIONI MOJA CHILE WAKOSA MAJI


Ni wazi mvua kubwa ambayo imenyesha nchini Chile na kusababisha mafuriko imewaacha wananchi wa nchi hiyo na shida ya kupata maji safi na salama kwani mafuriko hayo yamechafua maji katika vyanzo vya maji ambavyo walikuwa wakivitumia.
Mamlaka ya Maji ya mji mkuu wa Chile, Santiago imekiri kutokea kwa tatizo hilo na inafanya jitihada kurekebisha miundombinu na vyanzo vya maji ili waweze kuwasaidia wananchi wa mji huo ambao wanakadiriwa wananchi milioni 1.4 hawajapata maji safi na salama hadi sasa.
Licha ya watu hao ambao wamekosa maji safi na salama katika mji wa Santiago, pia zaidi ya watu milioni tano nchini humo wanaripotiwa kuathiriwa na mvua hiyo ambayo ilinyesha maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ya Amerika Kusini.
Madhara hayo yamekuja baada ya wikiendi kunyesha mvua kubwa ambayo imesababisha vifo vya watu watatu na wengine 19 wakiripotiwa kutokuonekana licha ya juhudi mbalimbali kufanywa na idara za ukoaji ili kuwapata.

0 Responses to “ZAIDI YA WANANCHI MILIONI MOJA CHILE WAKOSA MAJI ”

Post a Comment

More to Read