Tuesday, February 28, 2017

MLEVI ASASABABISHA MAJERAHA KWA WATU 28


Mtu mmoja ambaye inasemekana alikuwa amelewa sana pombe amesababisha watu zaidi ya 20 kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu ya haraka baada ya kuwagonga na gari kubwa.
Tukio hilo limetokea New Orleans, mjini Louisiana, Marekani wakati mtu huyo alipoingia katika moja ya mtaa uliopo katikati ya mji na kugonga magari matatu yaliyokuwepo kando ya barabara kisha kuwagonga watu waliokuwa eneo hilo.
Baada ya tukio hilo, watu 28 walibainika kupata majeraha na 21 kati ya kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya haraka na mmoja wa majeruhi akiwa ni askari Polisi.
Polisi Louisiana hawajatoa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo na zaidi wakisema kuwa kwa sasa wanachunguza tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumchunguza mtu aliyesababisha tukio.

0 Responses to “MLEVI ASASABABISHA MAJERAHA KWA WATU 28”

Post a Comment

More to Read