Monday, February 20, 2017
SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA GAMBIA,ADAMA BARROW
Do you like this story?
Mtangulizi
wa Adama Barrow aliwahi kuapa kwamba angetawala nchi hiyo ya Gambia
hata kwa miaka bilioni moja kama ikibidi. Yahya Jammeh alibwagwa kwenye
Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana lakini
akakataa kuachia madaraka mpaka pale majeshi ya nchi za Afrika Magharibi
zilipopeleka wanajeshi wake mpakani mwa nchi hiyo.
Sherehe hizi za uapishwaji wa Rais Barrow zimeenda sambamba na kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Taifa hilo la Afrika Magharibi.
Katika hotuba aliyotoa baada ya kuapishwa, Rais Barrow alielezea hali ngumu ya kiuchumi iliyopo nchini humo iliyosababishwa na mtangulizi wake, Yahya Jammeh.
“Tumerithi mdororor wa uchumi,” alisema na kuahidi kuvutia wawekezaji katika sekta ya teknolojia, kutoa bure elimu ya msingi na kuboresha mfumo wa utoaji na upatikanaji wa haki za wananchi kupitia mahakama.
“Gambia imebadilika kabisa. Wananchi wamezinduka kabisa na wanatambua kwamba wanaweza kuiingiza serikali madarakani na pia kuitoa kama wakitaka.”
Tazama hapa picha tisa za sherehe hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru nchini humo:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA GAMBIA,ADAMA BARROW”
Post a Comment