Monday, February 20, 2017
UKAME WASABABISHA WANANCHI KUCHANGIA CHAKULA NA MIFUGO YAO
Do you like this story?
Wakulima
nchini Kenya wameanza kuwalisha mifugo wao vyakula walivyohifadhi ili
kuwaokoa kutokana na ukame ulioathiri zaidi ya nusu ya Taifa hilo mpaka
sasa.
“Kama ukipata chai au uji unawagawia na mifugo yako, bila kufanya
hivyo watakufa. Tutafanya nini sasa? Tutakufa pamoja na mifugo yetu,”
mfugajo mmoja aliiambia BBC
Katika moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaskazini mwa mwa nchi
hiyo eneo la Marsabit, mizoga ya mifugo inaonekana kuzagaa na kuoza
katika maeneo ambayo yalikuwa ni malisho yao kabla ya ukame. Ng’ombe
ambao awali walikuwa mmoja anauzwa Shilingi milioni 1.2 kwa sasa ni
Shilingi 120,000 kwa sababu wamekonda kupita kiasi.
Serikali iliahidi kuinunua mifugo hiyo ili kuwapunguzia wananchi
athari za madhara ya ukame huo lakini wakulima hao wameiambia BBC kwamba
bafo mpaka sasa hilo halijafanyika. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
ametangaza kwamba ukame ulioikumba Kenya ni Janga la Taifa na ameomba
mashirika ya kimataifa na nchi za nje kuisaidia nchi hiyo.
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya linasema kuwa watu milioni
2.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula na maafa yakuwa makubwa endapo
msaada wa haraka hautatolewa. Wananchi wanatembea zaidi ya kilomita 10km
kufata maji. Vyanzo vya maji vimekauka, vichache vilivyobakia
havitoshelezi kwa mahitaji ya wananchi pamoja na mifugo yao.
“Kama mvua haitanyesha hivi karibuni, hili litakuwa janga kubwa.
Tutapoteza maisha, sio maisha ya mifugo ya wanyama safari hii, ila ni
maisha ya binadamu,” alisema mkuu wa Mamlaka ya kukabiliana na athari za
ukame nchini Kenya, Guyo Gulicha.
Hali hii imekuja kutokana na mvua kutonyesha kwa mwaka wa tatu
mfululizo hivyo kufanya wakulima na wafugaji kushindwa kumudu maisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UKAME WASABABISHA WANANCHI KUCHANGIA CHAKULA NA MIFUGO YAO”
Post a Comment