Tuesday, February 21, 2017

UNA TATIZO LA KUCHELEWA KUAMKA? TUMIA NJIA HIZI KUMI KUWAHI KUAMKA ASUBUHI


1.Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi, kwamba ukiamka asubuhi  tu cha kwanza ni kula chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii itakufanya Utoke kitandani pale tu atakaposhtuka!

2.Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya  zaidi iwe ya kwanza kutendeka asubuhi. Utajkuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi hiyo na siku yako itaenda vizuri

3.Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi jumatatu, andaa nguo ya kuvaa jumapili usiku. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40 (40%) ya watu huchelewa kutoka kitandani kwa kuwa walitumia muda mwingi kupanga watavaa nguo gani.


4. Anza kupunguza dakika 20 kila siku Taratibu; Kama ulikua unaamka saa mbili kamili, amka saa moja na dakika arobaini, baada ya siku mbili punguza tena dakika ishirini mpaka utakaporidhika

5. Jiwekee Lengo na uwaambie watu. Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii kwa kutaka kuwaonyesha watu kwamba umetimiza lengo lako na utajikuta unawahi kuamka asubuhi

6. Tengeneza “appointment” (Miadi) ya kuonana na mtu asubuhi, utajikuta unawahi kuamka kwa kuogopa kumuangusha mtu huyo.

7. Kama una mtu unaishi nae, tengeneza ratiba ya pamoja kama kufanya mazoezi, maombi, kusoma nk! Itakusaidia kukuongeza morali ya Kuwahi kuamka.

8 Weka saa ya kukuamsha (alarm clock)  mbali na kitanda ikiwa na sauti kubwa, ni vizuri ukitumia wimbo uupendao.

9. Muombe mpenzi wako akuamshe kila asubuhi, au jenga tabia ya kumpigia mpenzi wako simu asubuhi


10.Ondoa vitu Vinavyokufanya uchelewe Kuamka  mfano; pombe, kahawa na kuwahi kulala usiku.

0 Responses to “UNA TATIZO LA KUCHELEWA KUAMKA? TUMIA NJIA HIZI KUMI KUWAHI KUAMKA ASUBUHI ”

Post a Comment

More to Read