Friday, February 24, 2017
SIMULIZI MAUAJI YA KIBITI
Do you like this story?
Shuhuda
wa tukio la mauaji ya Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya
na maofisa wawili wa maliasili na utalii, Samwel Joseph amesema kifo
hicho kimekatisha ndoto ya askari huyo kuhakikisha amani inatawala.
Alisema
Kubezya alifanikiwa kurejesha nidhamu kwa polisi waliokuwa
wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa raia kama vya kuwakamata
vijana wanaobeba mbao kwa ajili ya kujitafutia riziki na kuwapora.
“Tumepoteza mpambanaji aliyelenga kuutokomeza ujambazi wilayani hapa unaozidi kuota mizizi kila kukicha,” alisema.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo, Daudi Siang’a alisema: “Alikuwa amedhamiria hasa
na ndiyo maana alijitoa kimasomaso kukabiliana na majambazi.”
Akizungumza
kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, WP Jesca, kutoka ofisi ya
habari ya polisi mkoani Pwani, alisema wanaendelea na uchunguzi ili
kuwatia mbaroni waliohusika katika mauaji hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMULIZI MAUAJI YA KIBITI”
Post a Comment