Friday, February 24, 2017
MAREKANI YASITISHA ZOEZI LA KUWARUDISHA MAKWAO RAIA WA KIGENI
Do you like this story?
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Rex Tillerson amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Mexico Luis
Videgaray mjini Mexico, mkutano ambao kwa kiasi kikubwa ulilenga
majadiliano kuhusu masuala ya sera za uhamiaji.
katika mkutano huo, Waziri wa mambo ya nje wa Mexico, Luis Videgaray amesema amechukizwa na sera za Marekani dhidi ya nchi yake.
Amesema kuwa US Secretary of state, Rex Tillerson na mkuu wa mambo ya
usalama , John Kelly kuwa mapendekezo ya marekani kuhusu masuala ya
uhamiaji yana madhara makubwa.
”Ni heshima kubwa na tunatoa shukrani kwa ujio huu, kwa kuwa
umefanyika kipindi kigumu kwa Mexico na Marekani.kama nyote mjuavyo,
kumekuwa na hali ya kutoridhishwa ,hali ya kukerwa na kile kinachoelezwa
kuwa sera ambazo zinaweza kuleta athari kwa maslahi ya raia wa Mexico
ndani na nje ya Mexico”
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Kelly amesema
hakutakuwa na zoezi la kuwarejesha makwao raia wa kigeni wanaoishi
kinyume cha sheria nchini Marekani na kuwa jeshi halitatumika kwenye
operesheni ya kuwarudisha nyumbani.
Naye Rais wa zamani wa Mexico, Vicente Fox ameonyesha wasiwasi wake
kuhusu utawala wa Trump kuwa umeharibu mahusiano mazuri yaliyokuwapo
kati ya Mexico na Marekani
Mawaziri hao wawili pia walikutana na Rais wa Mexico, Enrique Pena
Nieto, ambaye hivi karibuni alisitisha safari yake ya kukutana na rais
wa Marekani,Donald Trump, baada ya Trump kusisitiza kuwa Mexico ilipe
gharama za kujenga ukuta wa mpaka baina ya Marekani na Mexico
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAREKANI YASITISHA ZOEZI LA KUWARUDISHA MAKWAO RAIA WA KIGENI ”
Post a Comment