Friday, February 17, 2017
WATUMISHI WA TRA MBARONI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA
Do you like this story?
Vita dhidi ya Dawa za Kulevya vado inaendelea kushika kasi katika
maeneo mbalimbali ya nchini ambapo hadi sasa watu wengi tayari
wameshakamatwa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Simon Sirro alisema jana kuwa hadi sasa wanawashikilia watu 349 kwa
tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamishna wa Operesheni wa
Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya, Mihayo Msikhela ametoaa
ripoti ya operesheni iliyofanyika kwa siku nne Tanzania kote na kusema
kuwa wamefanikiwa kuwakamata watumishi wawili wa TRA wanaotuhumiwa
kupitisha kemikali badhirifu inayotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Kuhusu kuwataja majina, Kamishna Mihayo amesema kuwa si sahihi kuwataja kwa sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATUMISHI WA TRA MBARONI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA”
Post a Comment