Tuesday, May 2, 2017

AUDIO: ‘Ni vizuri matetemeko madogomadogo yaendelee kutokea’ -RC Kagera






Kufuatia tetemeko llililotokea kwa mara nyingine mkoani kagera majira ya saa 7 na dakika 29 za usiku wa kuamkia April 30 mwaka huu,mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa 3.1 vipimo vya ritchel.
Wanasema lile tetemeko lilitokea ziwani eneo la Minziro, zile ni after shocks za lile lililotokea mwaka jana mwezi wa tisa na wanasema ni vizuri yaendelee kutokea hayo madogomadogo kuipa nafasi miamba ipumue kuliko kukaa muda mrefu miaka na miaka alafu linatokea kama  lile la mwaka jana’RC Kijuu
Wanasema hizi after shocks zitakuwepo na zitaendelea kuwepo ni miamba inapumua,muhimu tuzingatie yale tuliyokuwa tunashauliwa na wataalamu mbalimbali wa miamba waliokuja na tuachane na taaruki‘-RC Kijuu

0 Responses to “AUDIO: ‘Ni vizuri matetemeko madogomadogo yaendelee kutokea’ -RC Kagera”

Post a Comment

More to Read