Wednesday, May 3, 2017

UEFA CHAMPIONZ LIGI: RONALDO HATARI, AIFYEKA ATLETICO 3 KWENYE EL DERBI MADRILENO HUKO BERNABEU!


>LEO MONACO v JUVENTUS!
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali – Mechi za Kwanza
Jumanne Mei 2
Real Madrid 3 Atletico Madrid 0
++++++++++++++++


JANA huko Estadio Santiago Bernabéu Jijini Madrid Nchini Spain Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Kwanza ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kati ya Mahasimu wakuu wa Mji huo Real Madrid na Atletico Madrid ambayo hubatizwa El Derbi Madrileno, ilichezwa na Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo aliibuka Shujaa kwa kubamiza Bao zote 3 wakati Real ikishinda 3-0.
Hii ilikuwa ni mara ya 5 kwa Timu hizi kupambana katika Mechi za Ulaya na Real Madrid walimaliza ndoto za Atlético Madrid kwenye UCL katika Misimu Mitatu iliyopita, ikiwa ni pamoja wa Fainali za Mwaka 2014 na 2016, na safari hii hali inaelekea ni hiyohiyo labda Atletico wamudu kubadilika katika Marudiano Wiki ijayo wakiwa kwao Vicente Calderon na kupindua kipigo hiki cha 3-0.
Ronaldo aliipa Real Bao lao la Kwanza Dakika ya 10 kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Casemiro na kupiga Bao nyingine 2 Dakika za 73 na 86.
Hii ni mara ya Pili mfululizo kwa Ronaldo kupiga Hetitriki kwani katika Mechi 2 zilizopita za Robo Fainali za UCL dhidi ya Bayern Munich alipiga Hetitriki kwenye Mechi hizo alizofunga Jumla ya Bao 5.
Ronaldo ndie Mfungaji Bora katika Historia ya UCL akiwa na Bao 103.
Hii Leo ipo Mechi nyingine ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UCL huko Monaco kati ya AS Monaco na Juventus.


VIKOSI:
REAL MADRID:
Navas, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo, Kroos, Casemiro, Modrić, Isco, Benzema, Ronaldo
Akiba: Casilla, Nacho, James Rodríguez, Kovačić, Vázquez, Asensio, Morata
ATLÉTICO MADRID: Oblak, Lucas Hernández, Savić, Godin, Filipe Luis, Koke, Gabi, Saúl Ñíguez, Carrasco, Griezmann, Gameiro
Akiba: Moyà, Tiago, Torres, Correa, Thomas, Gaitán, Alberto Rodríguez
REFA: Martin Atkinson [England]
UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI
Nusu Fainali – Mechi za Kwanza
**Mechi kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku, Saa za Bongo
Jumatano Mei 3
AS Monaco v Juventus
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

0 Responses to “ UEFA CHAMPIONZ LIGI: RONALDO HATARI, AIFYEKA ATLETICO 3 KWENYE EL DERBI MADRILENO HUKO BERNABEU! ”

Post a Comment

More to Read