Friday, March 21, 2014

AGIZO LA WAZIRI NYARANDU JUU KUPIGA MARUFUKU UVAAJI HERENI NA VIDANI VYENYE KUNAKISHIWA NA MENO YA TEMBO LAPOKEREWA TOFAUTI JIJINI.


Waziri wa Maliasiri na Utalii Ndugu Lazaro Nyarandu


Msanii wa sanaa ya Uchongaji na uchoraji wa vitu vya kitamaduni Ndugu Luchas Masanyika katika eneo la Sokoine Jijini Mbeya


Rasta Philip Kafuku muuzaji na msanii wa sanaa ya uchongaji na uchoraji eneo la jijini Mbeya.





Kufuatia hatua ya serikali kupiga marufuku uuzwaji na uvaaji wa bidhaa zenye kunakishiwa na Meno ya Tembo wadau mbalimbali jijini Mbeya watoa changamoto zao juu ya kufanikiwa kwa zoezi hilo.

Wakizungumza jijini mbeya baadhi ya wadau hao wamedai kuwa suala hilo ni zuri kwani  serikali ipo katika kutekeleza wajibu wake lakini bado suala la kuuwawa kwa tembo litabaki kuwa pale pale kama hakuta kuwa na uthubutu wa kupambana na majangiri na kubaini wahusika wa vitendo hivyo..


Mkazi wa Jakaranda jijini Mbeya Ndugu Philip Kafuku ambaye pia ni Msanii wa uchongaji na uchoraji amedai kuwa hatua ya serikali kupiga marufuku suala la uvaaji wa vidani au shanga zenye kunakishiwa na meno ya tembo bado halita weza kuzuia kuuwawa kwa tembo hao.


Amesema uvaaji wa vitu hivyo huana makosa yoyote badala yake serikali ijaribu kufanya utafiti wa kutosha wa  namna gani tembo hao wanauwa kila kukicha .


Amedai kuwa badala kupunguza tatizo kutaongezeka tatizo  kutokana na marighafi hizo kuwa adimu sokoni hivyo kuchangia   kuongeza  thamani yake.

  Kwa upande wake Ndugu Lucas Masanyika Mkazi wa Uhindini jijini humo amedai kuwa nivema serikali ikajipanga upya katika kudhibiti kuwawa kwa tembo hao  badala ya kuzuia watu kuvaa shanga na vidani vyenye kutengenezwa na meno ya tembo bila kujua mhusika mkuu wa mauji hao.

Amesema mvaaji hana makosa yoyote kwani yeye hununua  kutoka kwa mfanyabiashara hivyo upigaji marufuku huo  hakutosaidia chochote kupunguza tatizo hilo badala yake serikali ijipange katika kuongeza ulinzi katika maeneo ya mbuga za wanyama.


Hivi karibuni Waziri wa Maliasiri na Utalii Ndugu Lazaro Nyandu amepiga marufuku uvaaji na uuzwaji wa hereni na Shanga zenye kunakishiwa na meno ya Tembo kwa lengo la kuzuia tatizo la kuwawa kwa Tembo.


Nyarandu Alisema endapo mtu yoyote atabainika kukutwa na hereni au shanga zenye kutengenezwea na meno ya tembo atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria

0 Responses to “ AGIZO LA WAZIRI NYARANDU JUU KUPIGA MARUFUKU UVAAJI HERENI NA VIDANI VYENYE KUNAKISHIWA NA MENO YA TEMBO LAPOKEREWA TOFAUTI JIJINI.”

Post a Comment

More to Read