Friday, March 21, 2014

MTANDAO WA TWITTER KUFUNGWA.


Mtandao wa kijamii wa, Twitter, unafungwa nchini Uturuki, saa chache baada ya waziri mkuu, Recep Tayyip Erdogan, kuahidi kuuondoa.

Bwana Erdogan -- ambaye anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi aliwaambia maelfu ya wafuasi wake katika mkutano wa uchaguzi kuwa hajali kuhusu namna jamii ya kimataifa itakavyochukulia hatua yake.

Neelie Kroes, ambaye ni naibu rais wa tume ya muungano wa Ulaya amesema umamuzi wa kufungwa kwa mtandao huo ni wa kulaumiwa.

Serikali ya Bwana Erdogan imekuwa ikilalamika kuwa mtandao wa Twitter ulipuuza uamuzi wa mahakama ulioitaka viunganishi vya taarifa zake vinashukiwa kurekodi mawasiliano yake binafsi.

0 Responses to “MTANDAO WA TWITTER KUFUNGWA.”

Post a Comment

More to Read