Friday, March 28, 2014
BALOZI SEIF AMPONDA MAALIM SEIF.
Do you like this story?
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Idd ametangaza vita kwa mtu yeyote
anayepanga njama za kuvuruga mchakato wa Rasimu ya Pili ya Katiba.
Hata hivyo amebeza kauli ya makamu wa kwanza
wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad aliyoitoa juzi kwenye viwanja vya
Kibandamaiti Zanzibar akisema kuwa kiongozi huyo hana uwezo wa kufanya chochote
kisiwani humo.
Juzi katika hotuba yake Hamad alisema chama
chake hakiko tayari kuunga mkono suala la Serikali mbili na wala suala la
hotuba ya Rais Jakaya Kikwete bali wako katika misingi ya hotuba ya Jaji
Warioba.
“Mheshimiwa Hamad hana uwezo wa kufanya jambo
lolote visiwani Zanzibar. Zaidi ya yote ataishia kusema tu bila ya mafanikio na
ndiyo maana Wazanzibari wameshatambua kuwa mzee yule ni mwongo,” alisema Balozi
Idd.
Alisema hali ikiendelea hivyo na Serikali ya
Mapinduzi haitasita kuwashughulikia watu wote wa aina hiyo.
Kuhusu nafasi ya Makamu wa Kwanza alisema
kuwa alitoa kauli ile kwa nafasi yake ya katibu wa chama cha CUF, lakini hakuwa
amesimama kama makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu huyo alipinga kauli kwamba Wazanzibari
hawataki serikali mbili kwa kuwa hakuna aliyeulizwa juu ya jambo hilo.
“Kule Zanzibar tuko karibu watu 1.3 milioni,
sasa nani aliulizwa kama si uongo wa kutaka kuwagombanishwa watu. Wanafanya
ubaguzi usio na maana na hiyo ni choyo tu,” alisema.
Aliwataka wananchi wa Serikali ya Zanzibar
kupuuza kauli za makamu wa kwanza wa Serikali ya Zanzibar kwa madai kuwa kauli
zake ni kwa masilahi yake na chama chake.
Alisema kwa sasa inaonekana kuwapo na baadhi
ya wanasiasa ambao wana mpango wa kukwamisha mjadala wa kujadili Rasimu
ya Katiba, ikiwamo kikundi cha Ukawa.
Huku akionekana kuunga mkono hotuba ya
mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ina mashiko na ni nzuri
lakini akaponda suala la serikali tatu.
Aliwatupia lawama wanasiasa kuwa wamekosa
uvumilivu na utashi wa kweli katika kupata Katiba ya nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BALOZI SEIF AMPONDA MAALIM SEIF.”
Post a Comment