Friday, March 28, 2014
NDEGE YA MALAYSIA KUTAFUTWA ENEO LIPYA.
Do you like this story?
![]() |
Ndege 9 za kijeshi na Moja ya kiraiya zinatafuta mabaki ya ndege ya Malaysia ya MH370 |
![]() |
Eneo inakotafutwa ndege ya Malaysia
|
Maafisa wanaosaidia katika
harakati za kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu
yaliyopita , wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege
hiyo.
Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja
mia moja kazkazini mashariki mwa kusini mwa bahari hindi.
Mamlaka ya usalama wa baharini nchini
Australia imesema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa
Malaysia pamoja na matokeo ya utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.
Ndege hiyo iliyotoweka March tarehe 8 ikiwa
na abiria 239 sasa inadaiwa kwamba ilikuwa katika mwendo wa kasi kinyume na
ilivyokadiriwa na kwamba huenda iliishiwa na mafuta ghafla.
Meneja mkuu wa shirika la utafiti wa anga za
juu ya Australia John Young, amesema utafiti mpya unaonesha kuwa ndege hiyo ya
MH370 ilikwea juu na kufululiza kwa kasi mno na hiyo inaweza kuwasababu ya mafuta ya ndege hiyo kumalizika
haraka.
Kutokana na hesabu hiyo mpya eneo la kutafutwa kwa ndege hiyo imehamishwa hadi umbali wa kilomita 1,850 Magharibi mwa Perth na itakuwa katika eneo lenye kilomita 319,000 mraba katika bahari Hindi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NDEGE YA MALAYSIA KUTAFUTWA ENEO LIPYA.”
Post a Comment