Thursday, March 27, 2014
HATARI: WAFANYA BIASHARA WATEKWA NA MAAFISA USALAMA FEKI SINGIDA.
Do you like this story?
Na
Nathaniel Limu, Singida
WAFANYABIASHARA
wa Manyoni mjini mume na mke,wametekwa na watu watatu waliojifanya kuwa ni
maafisa usalama wa taifa makao makuu jijini Dar-es-salaam.
Waathirika
wa utekaji huo ni Methew Dominik @ Cheupe (46) na mke wake Selina Methew (42).
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo
limetokea juzi saa tisa alasiri Manyoni mjini.
Amesema
Faraja George (35) mfanyabiashara wa Dodoma mjini,mganga wa tiba asilia na
mkazi wa mkoa wa Tanga,Saidi Mgolola @Pesa mbili (49) Michael Peter na
Michael Peter (26) mkazi wa Moshi mjini na dereva wa gari lililotumika katika
utekaji huo.
Amesema
siku ya tukio watuhumiwa wakiwa na gari T.242 CBM aina ya toyota prado,walifika
dukani kwa Methew baada ya kudai kuwa wao ni maafisa usalama taifa,walimwamuru
mwenye duka kuwa wanamhitaji Singida mjini kwa ajili ya mahojiano.
“Methew
aliwaomba maafisa hao bandia kuwa aambatane na mke wake huko kwenye mahojiano
hayo.Baada ya waathirika hao kuingia ndani ya gari,gari hilo badala ya kuelekea
Singida mjini,lilibadili na kuelekea Dodoma”,amesema.
Kamwela
amesema bahati nzuri polisi Manyoni mjini walipata taarifa ya tukio hilo mapema
na wakawasiliana na wenzao wa Bahi mkoani Dodoma ambao walifanikiwa kuwanasa
watuhumiwa hapo kwenye kizuizi.
Amesema
uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo,ni watuhumiwa kutaka
kumwibia mali mfanyabiashara hiyo Methew.Uchunguzi zaidi bado unaendelea.
Kamwela
amesema kuwa mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani
kujibu tuhuma inayowakabili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HATARI: WAFANYA BIASHARA WATEKWA NA MAAFISA USALAMA FEKI SINGIDA.”
Post a Comment