Thursday, March 27, 2014
UONGOZI WA DAMPO WAAGIZWA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA.
Do you like this story?
Mkurugenzi Mtendaji wa Tirima Enterprises, Bw. Robert Ngeleshi akizungumzia changamoto na matatizo ya mawakala wa kusomba taka katika jiji la Dar ambao waliongozana na Mkuu wa mkoa kwenye ziara hiyo. |
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ametoa agizo mara moja kwa uongozi
wa Dampo nje kidogo la jiji la Dar, Pugu Kinyamwezi, kurekebisha miundombinu ya
barabara pamoja na taa ili kurahisisha umwagaji wa taka katika dampo hilo.
Akizungumza na baadhi ya viongozi wa wilaya na
jiji hivi karibuni baada ya kufanya ziara ya ghafla katika maeneo kadhaa ya
jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa amesema tatizo la miundombinu ya barabara
kuelekea katika Dampo la Pugu Kinyamwezi linasababisha foleni kwa malori ya
kusomba taka katika jiji la Dar.
“mara
ya mwisho wakati nakuja hapa kukagua hili dampo kulikuwa na taa na kazi ilikuwa
inafanyika usiku na mchana sasa kumetokea nini,” alihoji Mkuu huyo wa Mkoa
Sadick
aliagiza kwa viongozi wa jiji kushughulikia haraka tatizo la miundombinu ya
barabara kuelekea Dampo ili kuongeza tija katika kazi ya kumwaga na kusomba
taka katika jiji la Dar es Salaam.
Alisisitiza
kwamba utaratibu mbovu wa umwagaji taka na miundombinu mibovu katika Dampo la
Pugu Kinyamwezi vinasababisha mrundikano wa taka katika manispaa zote za
Temeke, Ilala na Kinondoni.
Amesema
kwamba ni muhimu kwa viongozi wa jiji kupata nguvu kazi ya kutosha ili kuwe na
watu watakaosimamia umwagaji wa taka wakati wa usiku ili kudhibiti madereva
wakorofi wanaomwaga taka ovyo bila kuzingatia taratibu.Sadick aliongeza kuwa watendaji wa jiji ni lazima
wawe na utaratibu wa kutoa mafuta kwa wakati kwenye magari ya kusomba (Bull
Dozer) na vitendea kazi vingine.
Wakati
akitembelea maeneo kadhaa kati kati ya jiji kuanzia soko la Kisutu na mitaa ya
Libya, Mkuu wa Mkoa aliagiza mamlaka zinazohusika kushughulikia haraka tatizo
la maji machafu kupunguza harufu na kuzuia magonjwa ya mlipuko. “nawaagiza mkae pamoja na mje na mpango mkakati
utakaowezesha kumaliza tatizo la maji machafu yanayotoka katika mitaro na
mifereji ya maji machafu katika ya jiji,” aliongeza.
Wakati
huo huo, wadau kadhaa wa usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam wameomba
serikali kutoa kipaumbele kwa Dampo la Pugu Kinyamwezi na kulitengea bajeti ya
kutosha ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UONGOZI WA DAMPO WAAGIZWA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA.”
Post a Comment