Thursday, March 27, 2014

MAOFISA USALAMA WAMWANGWA MIKUTANO YA KAMATI ZA BUNGE.




Ofisi ya bunge la katiba imeweka maofisa usalama katika kumbi zote zinazotumika kufanya vikao vya kamati.


maofisa usalama  wapatao wanne wakiilinda  katika kumbi zilizoko  katika hoteli ya Dodoma  ambako kamati namba  tano na sita zinafanya vikao.

Katika kumbi zilizopo st gasper pia hali ilikuwa  hivyo nako kulijaa  maosifa usalama  na polisi wanaoendelea kulinda  kumbi mbili zinazotumika kwa mijadala hiyo.

Tumeenda pale hatukuruhusiwa  kukaa katika mabembea hali ambayo ilitufanya kushindwa hata  kupata picha za uchaguzi wa mwenyeviti na makamu  alisema mmoja  wa wapiga picha wa magazeti.

Awali mwenyekti wa bunge Samuel sitta aliwatangazia wajumbe wa bunge hilo kuwa kutakuwa na ulinzi katika kumbi zote za kamati  aliwataka wajumbe  hao kuvaa vitambulisho vyao  wakati wote wanapokuwa  katika kumbi hizo ilii maofisa usalama waweze kuwatambua.

0 Responses to “MAOFISA USALAMA WAMWANGWA MIKUTANO YA KAMATI ZA BUNGE.”

Post a Comment

More to Read