Thursday, March 27, 2014

MJUMBE AMPA SOMO MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA.





Mjumbe wa bunge la katiba  constatine akitanda ameshauri mwenyekiti  wa bunge la katiba  Samuel sitta azibe masikio kwa chama chake ili aweze  kulipeleka taifa mahali salama.

Akitanda amesema hayo katika mahojiano  maalumu  yaliyofanyika Dodoma  juzi.

Kwa jinsi sitta  anavyoliendesha  bunge hilo asifikiri kuwa ni njia sahihi bali anachochea wajumbe hasira wakati  katiba ni suala  la maridhiano alisema.

Mwenyekiti anayo nafasi ya kulpeleka taifa mahali salama  kwa kuziba masikio  kwa chama  chake najua ni vigumu lakini inawezekana  kufanya hivyo kwa kuendesha bunge  kidemokrasia.

Alimtaka sitta akumbuke kuwa mapendekezo  ya katiba yatapelekwa kwa wananchi  kwa ajili ya kupigiwa kura na kwamba wananchi wanajua pumba na mchele ni ufupi kwa sababu wanaona na kusikia.

Ni heri majina yetu yaandikwe kwa masizi yafutike baada ya muda mfupi kuliko kukubali  kuburutwa  na majina kuandikwa kwa wino wa dhahabu alisema akitanda.

Kuhusu muundo wa serikali akitanda alisema  ni ukweli kwamba Tanzania  kumekuwa na kero za muungano  kwa miaka 50 ambazo hazijatulika lakinijambo la kujiuliza ni kama seikali tatu ama mbili zinatoa majibu.

0 Responses to “MJUMBE AMPA SOMO MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA.”

Post a Comment

More to Read