Thursday, March 27, 2014

MKENYA ATUHUMIWA KUIKOSESHA MAPATO TCRA.


Raia wa Kenya nelson rading onyango amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi  kisutu  dare s salaam  akikabiliwa na mashitaka saba  ikiwamo la kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila ya kuwa na leseni  na kulisababisha taifa hasara ya zaid y ash 6.8 bilioni.

Akisomea hati ya mashtaka wakili mwandamizi wa serikali tumaini kweka alidai  jana kuwa kati ya julai 2010  na November 2013 katika eneo la kariakoo mshitakiwa  alifanya udanganyifu matumizi ya mtandao kinyume cha sheria.

Kweka alidai kuwa mshtakiwa kwa nia ya udanganyifu alikuwa akiendesha huduma za mawasiliano  ya kimtaifa huku akikwepa kutumia njia halali za malipo zinapotolewa na mamlaka  ya mawasiliano Tanzania(TCRA)

Katika shitaka la pili  anadaiwa  kutoa huduma  ya mawasiliano  bila ya kuwa na leseni wakili huyo wa serikali alidai kuwa katika kipindi hicho mshtakiwa bila ya kuwa na uhalali kisheria alito a huduma ya simu za kiamtaifa  bila ya kuwa na leseni inayotolewa na TCRA .

Katika shitaka la tatu anadaiwa kuwa kati ya January 2013  na November 2013 akiwa katika eneo la kariakoo alitumia kadi  za simu zisizo  sajiliwa.

Katika shitaka la nne anadaiwa kuingiza nchini vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu  kufanya hivyo.

Katika shitaka la tano alidai kuwa licha ya kuingiza nchini mitambo hiyo bila ya kuwa na kibali mshitakiwa  huyo alisimika mitambo mine ya mawasiliano na kuiendesha. Mitamgo hiyo ni SM boxi zenye namba za siri TX 2SN5600C5/05,TX2SN48002/K21,TX2SN1002335A na cisco router.

Katika shitaka la sita wakili alidai kuwa onyango alitumia mitambo hiyo  ya kielektroniki  ambayo ilikuwa haijathibitishwa  na TCRA .

Mshtakiwa pia anadaiwa  kusababisha hasara y ash 6.8 bilioni kwa TCRA kati ya julai 2010  na November 2013 kwa kutoa huduma za mawasiliano  ya kimataifa bila ya kuwa na leseni.

0 Responses to “MKENYA ATUHUMIWA KUIKOSESHA MAPATO TCRA.”

Post a Comment

More to Read