Thursday, March 27, 2014

NILIMHUDUMIA TUPPA KWA DAKIKA 25.




Mganga mkuu wa hospitali ya halmashauri  ya wilaya ya tarime marco  nega amesema  walimpokea mkuu wa mkoa wa mara  john tuppa akiwa mahututi  na alifariki dakika 25 za matibabu.

DK nega alisema tayari walikuwa  wamejiandaa kumpatia  matibabu  kwa sababu  walipewa taarifa mapema kwamba hali yake ni mbaya  baada ya kubadilika ghafla,  akipewa taarifa  na mkuu wa wilaya ya tarime john henjewele.

Amesema  walimpokea tuppa saa 3:45  asubuhi  na kwamba baada ya mapokezi walichukua vipimo na kukuta ni shinikizo la damu likiwa juu kwa kiwango  cha 160/ 140.

Kwa mujibu wa mwanasanyansi wa tiba ya binadamu Samuel shita kiwango cha peresha cha 160/140 mmhg ni  shinikizo  kali la damu.

Uhatari huo anauelezea ni mbaya zaidi kutokana na namba ya chini 140 ambayo kwa kawaida  inapaswa  kuwa kati ya 60 na 90.

Dk nega alisema wakati wakiendelea kujaribu kushusha shinikizo hilo kali ilipotimu saa 4:15 asubuhi alifariki dunia.

Tulipigiwa  simu kutoka ofisi ya DC(Mkuu wa wilaya) kuwa mkuu wa mkoa  analetwa kwa matibabu  tukijiweka tayari  kwakweli alifikishwa  akiwa mahututi  hajitambui alisema DK nega na kuongeza alikutwa (Tuppa) na shinikizo la damu iliyokuwa juu kwa hiyo tulimpokea akiwa mzima angekuwa amekufa tusingebaini ugonjwa huo maana mtu aliyekufa vipimo havionyeshi.

Baadhi ya wajumbe walikuwa kwenye kikao walieleza kuwa mkuu wa mkoa wakati anasomewa taarifa ghafla  hali yake ilibadilika na kuanguka chini ka kutokwa na mapovu mdomoni.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya ulizni na usalama alisema tuppa alikuwa mzima lakini walishangaa ghafla akiwa mekaa kwenye kiti alianza kuhema kwa nguvu kabla ya kuishiwa nguvu.


Katibu tawala mkoa wa mara bendicto ole kuyan ametoa ratiba awali ya kusafirisha na mazishi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa mara john tuppa.

Ratiba hiyo inaonyesha mwili huo utaagwa leo nyumbani  kwake ikulu ndogo  musoma kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi 3:20 asubuhi.

Kuyan amesema baada ya kuagwa saa 3:25 asubuhi mwili utapelekwa kanisani katoliki  jimbo la musoma kwa ajili ya ibada ya wafu itakayongozwa  na askofu  Michael msonganzila.

Amesema baada ya ibada saa 5:00 asubuhi  mwili utasafirishwa  kuelekea uwanja wa ndege mwanza  kwa ajili ya kuelekea Dodoma.

Kuyan amesema kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 6:00 mchana viongozi na wnanchi wa Dodoma wataaga mwili huo kutokana viongozi  kuokba kuaga hapo kwa asababu aliwahi kufanya kazi Dodoma.

Ameseme machi 29 kuanzia saa 3:00 asubuhi itafanyika ibada nyumbani kwake kilosa  na wananchi kuaga mwili kasha kupelekwa eneo la maziko.

0 Responses to “NILIMHUDUMIA TUPPA KWA DAKIKA 25.”

Post a Comment

More to Read