Monday, March 31, 2014
KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA MARA MOJA MPANDA.
Do you like this story?
Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Makamu wa Rais, Sasi Salula amefanya ziara ya kutembelea miradi
inayofadhiliwa na ofisi yake katika ukanda wa Ziwa
Tanganyika Wilayani Mpanda Mkoani Katavi na kujionea hali halisi ya
miradi inavyoendelea kutekelezwa na kagiza kukamilika mapema
iwezekanavyo.
Agizo hilo
amelitoa baada ya kukuta baadhi ya miradi ikiwa katika hali isiyoridhisha na
kupata hofu kama inaweza kukamilika kwa wakati ili kwenda sawasawa na mkataba
na wafadhili, hivyo akaagiza zichukuliwe hatua za haraka kukamilisha
miradi hiyo kabla ya muda kuisha.
Miradi hiyo
inasimamiwa na program ya uendelezaji na Uhifadhi
mazingira wa Bonde la ziwa Tanganyika katika mikoa ya Kigoma, Rukwa
na Katavi , na makao makuu ya miradi hiyo iko mkoani kigoma na ofisi ya makamu
wa Rais ndiyo inayosimamia .
Amesema watu
wanaoishi Nchi zinazozungukwa na ziwa Tanganyika wanakaribia karibu
milioni kumi, na wanakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira,
hivyo hatua za makusudi zisipochukuliwa kuhakikisha mazingira ya ziwa
hilo yanahifadhiwa huenda uchumi wa wananchi hao hasa wale wanaotegemea ziwa
Tanganyika ukawa mashakani.
Aliitaja miradi ya
inayotekelezwa kwa upande wa mkoa wa Katavi Katika wilaya ya Mpanda
, ukanda wa Ziwa Tanganyika kuwa ni miradi ya Elimu , Afya,
Maji na Ujenzi wa Mwalo unaojengwa kwenye kijiji cha Ikola Kata ya Ikola kwa
thamani ya shilingi milioni 800, fedha zilizotolewa na wafadhili kwa
ajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi wanaozunguka ukanda huo.
Akiwa katika Kijiji
cha Ikola kukagua ujenzi wa Mwalo ameitaka Halmashauri kusisimamia ujenzi wa
mwalo huo na kukamilika mara moja kabla ya muda uliopangwa na
wafadhili kumalizika.
Mkandarasi anayejenga
mwalo ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kazi iliyofanyika
hadi hapo ilipofikia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko la kuuuzia samaki,
na maeneo mengine muhimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AAGIZA MIRADI KUKAMILIKA MARA MOJA MPANDA.”
Post a Comment