Wednesday, March 12, 2014

KURA BADO KITENDAWILI BUNGE LA KATIBA.




Wakati wajumbe wa bunge maalumu la katiba wakipitisha rasimu ya kanuni za kuendesha bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa bikao rasmi vya bunge hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa takribani  wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi nay a siri.

Hata hivyo wajumbe wawili wa bunge hilo, mchungaji Christopher mtikila  wa DP na felix mkosamali wa NCCR – Mageuzi walisusia kupitisha azimio la kukubali kanuni za bunge hilo wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye umoja wa katiba ya wananchi (ukawa)

Kinana asema
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi, Abdulrahaman Kinana amesema pamoja na malumbano makali yanayoendelea katika bunge la katiba  anaamini sasa katiba itapatikana.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana mjini Dodoma kinana alisema haoni tatizo katika malumbano hayo na kwamba anaamini yanatokana na mitazamo tofauti ya makundi wanayotoka wajumbe.

Pale kila kundi lina msimamo wake iwe chadema, CUF, NCCR mageuzi, CCM na  hata makundi katika kundi la wateule wa Rais. Ilikuwa ni lazima kushuhudia mivutano ya aina hiyo. Amesema kinana na kuendelea : lakini mwisho wa yote nawaasa wjumbe kuwa na moyo wa kuvumiliana kwa sababu lazima kila kundi litetee hoja zake kulingana na  tathmini yake juu ya mwenendo wa siasa na matarajio yake ya baadaye.

Amesema kwa msingi huo, haoni tatizo kwa CCM kuweka misimamo katika baadhi ya hoja, ingawa chama hicho pia hakitasita kulinganisha nguvu ya hoja zake na hoja za wengine

0 Responses to “KURA BADO KITENDAWILI BUNGE LA KATIBA.”

Post a Comment

More to Read