Wednesday, March 12, 2014

MREMA: KURA YA SIRI NI UNAFIKI.





Mwenyekiti wa chama cha TLP . Augustino Mrema amesema watu wnaotaka kura ya siri bungeni ni wanafiki huku waziri wan chi katika ofisi ya Rais (mahusiano na uratibu) Stephen wassira akiahidi kuonyesha wazi msimamo wake na kwamba ukiathiri ustawi wa taifa nataka aadhibiwe angali hai au mfu.

Wakizungumza kwenye mahojiano na TBC jana mrema na wassira waliema wao wanataka kuonyesha msimambo wao.

Mrema amesema wajumbe wanaotaka kura ya wazi kwa kisingizio cha kuhofia kushughulikiwa na vyama vyao ni wanafiki na kuwataka waige mfano wake.

Naye wasira amesema hakuna sababu inayoweza kuhalalisha kura ya siri katika kuamua mambo nyeti kitaifa kama kuunda na kupitisha katiba mpya.

Amesema kama ni suala la msimamo wa mtu kutofautisana  na ule wa chama au kundi lililomweka  kwenye nafasi hiyo, ufahamika kupitia kwenye mijadala yake  ndani ya bunge katmati au katika mazungumzo yake ya kawaida.

Mimi msimamo wangu ni serikali mbili kwa sababu ni wenye historia inayoeleweka kuwa una dhamira ya kuunda mfumo wa muungano endelevu na nyingine nyingi zilizo nujeam kwa watu wote , nitasimamia  msimamo huo na  ikitokea  ukaleta madhara kwa taifa, hata nikishakufa watoto na wajukuu wangu waje tu kwenye kaburi langu , wanichape viboko, alieleza wassira.

0 Responses to “MREMA: KURA YA SIRI NI UNAFIKI.”

Post a Comment

More to Read