Thursday, March 13, 2014

MBEYA CITY YATENGA SH 40 MILIONI KWA AJILI YA POINTI SITA.


Kikosi cha Timu ya Mbeya City

MBEYA CITY inatarajia kutumia karibu sh 40 milini  ili kupata pointi sita katika mechi mbili za ligi kuu bara zitakazocheza jijini Dar es salaam  dhidi ya JKT Ruvu na Ashanti  United kwenye uwanja wa chamazi  complex Mbagala.

Kiasi hicho kitatumika kwa usafiri na malazi kwa ajili ya kikosi chake kinachoshika  nafasi ya pili  katika msimamo  ligi hiyo kwa kuwa na pointi 39 ilizozipata katika mechi 21.

Timu hiyo italazimika kusafiri hadi Dar es salaam na kucheza na JKT Ruvu  machi 22 halafu itarudi mbeya  kucheza na Prisons machi 30 kisha itaenda Dar es salaam tena kucheza na Ashanti April 5.

Timu hiyo ingeweza kupunguza nusu gharama hizo endapo ratiba ingeruhusu kubaki dare s salaam kucheza mechi hizo.

Mbeya City ambayo mara nyingi hutumia usafiri wa ndege, inatumia kati  ya sh 14 milioni hadi sh 20 milioni kwa safari moja ya kwenda dar es salaam na kurudi mbeya.

Akizungumza na Fahari News katibu mkuu wa timu hiyo Emmanuel Kimbe amesema gharama hizo ni kubwa kwao hakini hawana namna kwa vile wanahitaji pointi hizo kwa udi na uvumba.

“Kama tungecheza mechi za Dar es salam kwa wiki moja ingekuwa nafuu kwetu. Kwa mfano tungecheza jumamosi na mechi nyingine  ikawa jumatano.” Amesema.

“Ombi letu kwa wapangaji wa ratiba ni vyema wakaangalia  namna ya kuzipunguzia gharama timu ndogo. Hebu tazama sisitunatumia karibu sh 40 milioni katika mechi mbili tu, kama mambo haya ya ratiba yakirekebishwa mzigo wa gharama utapungua.   

0 Responses to “MBEYA CITY YATENGA SH 40 MILIONI KWA AJILI YA POINTI SITA.”

Post a Comment

More to Read