Thursday, March 13, 2014
WALIONUNUA IPTL SASA WAFUNGUKA.
Do you like this story?
Dar es salaam. Sakata la
ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya IPTL, limeibuka katka sura mpya baada ya
ya kampuni ya Pan Africa Power Solution
Ltd (PAP) kutetea ununizi huo.
Mwenyekiti mtendaji wa PAP
Harbinder Singh Seth aliibuka juzi mbele ya wandishi wa habari akisema ununuzi
wa mitambo hiyo ilikuwa biashara safi isiyokuwa na tatizo lolote kwa kuwa
alifuata sheria na kanunu husika.
“Nilifuata taratibu zote,
sikuja Tanzania kuchuma fedha, ninataka kuisaidia Tanzania kupata umeme wa
uhakika ambao ni muhimu kwa ukuaji wa
uchumia amesema seth.
Jumatatu iliyopita Fahari
News iliripoti kwamba kati ya Novemba 28 na desemba 8 mwaka jana PAP ilikabidhiwa dola za amrekani 122 milioni
(Sh 201 bilioni) zilizokuwa katika akaunti ya Escrow katika benki kuu ya Tanzania (BOT)
Akaunti hiyo ilifunguliwa
BOT ili kuhifadhi fedha ambazo Tanesco ilistahili kulipa IPTL kama gharama za uendeshaji , bbad ya kutokea
mgogoro ambao ulizalimisha peande husika
kupelekana mahakamani .
Wiki iliyopita Fahari News
iliandika kwamba fedha hizo zilitolewa
baada ya serikali kuamua kumaliza shauri hiyo na hapo ndipo fedha hizo
zilipochukuliwa katika akaunti hiyo ya PAP.
Hata hivyo, pamoja na seth
kukubali kuchukua fedha hizo amesema fedha zilikuwamo ni sh 150 billioni, huku
akitetea hatua hiyo ya ununizi wa IPTL
kwamba siyo kinyumbe cha sheria.
Kabla ya kuuzwa PAP, IPTL
ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya mechmar corporation ya Malaysia (asilimia
70) na VIP Engineering na Marketing Company limited ya Tanzania iliyokuwa na asilimia 30 .
PAP ni kampuni ya tatu
katika mgogoro huo kujitokeza na kutoa ufafanuzi tangu habari zake zilipoanza
kuandikwa. Kampuni ya kwanza ilikuwa ni VIP Engineering ya James Rugemalira na
baadaye akaibuka mwanasheria wa IPTL na wote walitetea mauzo hayo.
PAP ilivyonunua IPTL
Wakili wa PAP joseph
mwakandege alisema kwa miaka mitano ya IPTL iliendeshwa bila kuwapo kwa mgogoro
lakini baadaye iliibuka mivutano miongoni mwa wanahisa iliyosababisha
kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow.
Mwakandege alisema 2010,
sethi aliwasilisha nyaraka mahakamani kuonyeshakwamba alipewa mamlaka ya
kusimamia mali zote za mechamar hapa nchini.
Amesema baadaye sethi
alinunia hisa zote ambazo awali mechmar alikuwa ameuza kwa piperlink na
kuzihamishia PAP.
Kwa mujibu wa wakili huyo,
sethi baadaye alinunua asilimia 30 zilizosalia, na tayari mmiliki wa VIP,
Rugemalira amekwishakiri kupokea dola za
marekani 75 milioni (sh 120 bilioni) alizoziita kuwa ni fedha za ugoro.
Amesema baada ya mauzo
hayo, VIP ilikwenda mahakamani na kuomba kesi zote zinazohusu kampuni hiyo ya mechmar zifutwe.
September 5, mwaka jana
mahakamani iliamua kufuta kesi hizo hivyo PAP akapata haki ya mumiliki mali
zote za IPTL, ikiwa ni pamoja na fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow.
Mwakandege alisema baada
ya uamuzi huo, PAP ilikubali kulipa madeni yote ya IPTL na ufilisi wa muda
uliokuwa umewekwa kwa kampuni hiyo
iliondolewa.
Kutokana na hali hiyo
ilibidi kusainiwa mkataba kati ya IPTL na serikali kupitia wizara ya nishati na madini ifahamike kwamba akaunti ya Escrow
ilikuwa mali ya wanahisa wa IPTL haikuwa
na fedha walipokodi wala fedha za Benki
ya Standard Chartered ya Hong Kong
(Mkopeshaji wa IPTL) alisema mwkandege.
Alifafanua kuwa, serikali
ilitaka PAP kusaini makubalino kwamba iwapo watatokea wadai kwapya wa IPTL
itawalipa. Amesema baada ya hapo serikali
aliandika barua kwa BOT kuitaka iruhusu fedha hizo zilipwe kwa PAP.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIONUNUA IPTL SASA WAFUNGUKA.”
Post a Comment