Thursday, March 13, 2014

PRODUCER MSWAKI KUTUMIA STAILI YA MAREHEMU NGWEA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA MAMA MZAZI WA MAREHEMU .




Producer wa muziki wa anayejulikana kwa jina la Mswaki Kutoka studio ya Black Curtains amesema wiki hii anatarajia kuelekea mjini Morogoro kwa Mama Albert Mangwea kuchukua kibali cha kufanya style ya wa mwanae kibiashara. page 

 Akizungumza na Fahari News Leo Mswaki, amesema kuwa hataki kuwa na maswali mengi juu ya kutumia style hiyo ndio maana ameamua kwenda kwa Mama Mangwea. "Kwa upande mwingine kama mzazi anaweza akaona sio sahihi,sijui labda, so sitaki niwe na maswali mengi sana nikaona kwamba ninaweza nikaenda Morogoro kuongea na mama yake ni msikie yeye anasemaje, nikamsikilizishe nyimbo na nini," alisema producer huyo. 

"Mimi ninavyo hisi hiki kitu kinaweza kuwa na faida gani kwa muziki wa Albert na yeye aone kama ataona sawa aseme kama ni sawa ninaweza nikaendelea kuifanya au kama sio sawa. So kama akisema ni sawa mimi nitajua naipush kwa ukubwa gani kunzia ila nataka kwanza nimsikie yeye mwenyewe binafsi. 

Familia ita benefit percent nitagawa percent sijajua mpaka sasa hivi ni percent ngapi? Iwe 50,50, mimi nitagenga some of my time nitapanga ratiba yangu vizuri tu ya kazi zangu zisiingiliane kwasasabu huko itabidi ni act kama msanii sasa unajua kuna ma interview, shows kuna nini ,na upande mwingine mimi ni music producer kwahiyo itabidi nipange ratiba yangu sawa niko radhi kuipanga ratiba yangu kihivyo ili tu hiki ninachokifanya kifike pale ambapo mimi naona ni sawa ni sehemu sahihi"

0 Responses to “ PRODUCER MSWAKI KUTUMIA STAILI YA MAREHEMU NGWEA BAADA YA KUPATA KIBALI CHA MAMA MZAZI WA MAREHEMU .”

Post a Comment

More to Read