Thursday, March 13, 2014

WATOTO WAWILI WA KIKE WATENGWA NA FAMILIA MARA BAADA YA KUFIWA NA WAZAZI MMOJA WAO NI MLEMAVU .


Watoto hao Elebia Bonifasi( 13) na Iren Bonifasi( 12) wakiwa katika ofisi za Ofisa Mtendaji Kata ya Nzovwe jiji Mbeya kwa lengo la kutaka msaada zaidi waweze kulejea shule.

Mtoto Elebia akionyesha mguu wake ambao umekuwa ukimpa shida kwa muda mrefu sasa ambao umekuwa ukijaa na kuwa mkuba  mara umri wake unavyo zidi kuongezeka.


Nyumbani kwa dada yeo ambapo kwa sasa wanaishi watoto hao eneo la Nzovwe jijini mbeya.

Dada wa watoto hao Bi.Subi Bonifasi akizungumza kwa masikitiko makubwa juu ya hali inayo wakumba wadogo zake pamoja na maisha yake kwa ujumla.mara baada ya kufiwa na wazazi wao
Vitendo vya kikatiri na unyanyasaji kwa watoto bado vimeendelea kulikumba jiji la Mbeya ambapo katika hali isiyokuwa ya kwaida wanafunzi   wawili wa kike  Mmoja wao akiwa ni mlemavu wa mguu wa darasa la saba katika  shule ya msingi ya Jitegemee Nzovwe Iliyopo Jijini Mbeya wameshindwa kuendelea na elimu hiyo  baada ya kuondokewa na wazazi wa pande zote mbili huku  mlezi aliyechukua jukumu la kuwatunza  kudaiwa  kuwakatisha masomo na kuwatumikisha   mashambani.

 Wanafunzi hao ambao ni Elebia Bonifance (13) na Iren Bonifance (12) wote ni wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Jitegemee wameshindwa kuendelea na masomo hayo katika kipindi cha miezi mitatu baada ya wazazi wao kufariki.

 Akizungumza naFahari News wakiwa katika ofisi za Mtendaji Kata ya Nzovwe watoto hao ambao mmoja  kati yao Elebia Bonifance kupatwa na ugonjwa wa mguu wake mmoja kukua  kila mwezi licha ya kukatwa vidole vyake viwili ambavyo vinadaiwa kugundulika kuwa na tatizo la tezi.

 Akisimulia maswaiba ya ugonjwa wa mguu huo, mtoto Elebia amesema kuwa  alizaliwa akiwa amevimba vidole hivyo viwili vya mguu wa kushoto na kila alipokuwa anakua na vyenyewe viliendelea kukua  na kuzidi umri wake ndipo mama yake alipoamua kumpeleka hospitali na kukatwa akiwa na umri wa miaka tisa.



 Amesema, baada ya kukatwa vidole hivyo kidonda kilikauka lakini cha ajabu ni kwamba mguu huo unaendelea kuvimba hasa nyakati za mchana kutokana na kupigwa na jua lakini maumivu  hayasikii.



 Amesema,  maisha wanayoishi yeye na mdogo wake ni ya tabu sana kwani  mara baada ya mama yao kufariki walichukuliwa na baba yao mkubwa waliomtaja kwa jina la James ambaye ameoa wanawake wawili hivyo wao kuishi na mama yao mkubwa ambaye amekuwa akiwatumikisha kazi mashambani.

 Amefafanua kuwa wakati  wanachukuliwaa waliwaeleza kuwa  watawapeleka shule lakini mpaka sasa wanashangaa kila siku zinavyozidi shuleni hawaoni dalili zozote huku  mama mkubwa wao akichukua jukumu la kuwapeleka   shambani kulima tena bila ya kula hali ambayo iliwarazimu kutoroka.

 Amesema, akiwa shambani  mguu wake ulikuwa ukimuuma sana kutokana na jua hivyo mdogo wake kumuonea huruma na kumtaka watoroke na kurudi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi marehemu mama yao ambayo alipewa na rafiki yake kujihifadhi

0 Responses to “WATOTO WAWILI WA KIKE WATENGWA NA FAMILIA MARA BAADA YA KUFIWA NA WAZAZI MMOJA WAO NI MLEMAVU .”

Post a Comment

More to Read