Thursday, March 13, 2014
MTIKILA : HIVI MWENYEKITI HUNA HOFU YA MUNGU.
Do you like this story?
Mchungaji Christopher Mtikila |
Mchungaji Christopher
Mtikila ametuhumu mwenyekiti wa muda wa bunge maalum la katiba , pandu ameir
kificho kwamba hana hofu ya Mungu kwa kumnyima haki yake ya kuzungumza bungeni.
Hayo yalitolewa juzi
asubuhi wakati wajumbe wa bunge maalum wakipitisha azimio la kuridhia rasimu ya mwisho ya kanuni za bunge hilo.
Kanuni hizo zilipitishwa kwa kauli moja juzi baada ya mwenyekiti wa kamati ya kushauri na kutoa mapendekezo juu ya maboresho ya rasimu ya kanuni profesa
costa mahalu kuwasilisha hoja ya
kupitisha azimio hilo bungeni.
Wajumbe 13 kutoka karibu
kila kundi lililohusika kuunda bunge hilo, walizungumza kwa idhini ya kificho ,
ndipo baada ya mchangiaji wa mwisho
askofu amos mwagache kumaliza na
kificho kuanza kuhitimisha mjadala huo, ikaibuka sauti kutoka ndani ya ukumbi
huo.
“Mwenyekiti kwanini
unizuia kuzungumza? Niliyonayo hayawezi kunufaisha nchi? Nataka uniambie
kwanini unaninyima haki yangu? Haki inatajwa sana hapa ndani hata amri ya Mungu inahimiza kutenda haki hun
ahofu ya Mungu ndiyo maana unaninyima haki yangu” alisema mchungaji Mtikila na
kuongeza:
“Mwenyekiti unataka
wajumbe wazungumze unayotaka kusikia hii ni kumkosea Mungu kusema ni haki yangu
na mimi nina neno la kusema niache
nizungumze.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTIKILA : HIVI MWENYEKITI HUNA HOFU YA MUNGU.”
Post a Comment