Thursday, March 13, 2014
WABAYA WAMENIZUSHIA UGONJWA, ASEMA SITTA.
Do you like this story?
Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta |
Waziri wa ushirikiano wa
Afrika Mashariki Samuel Sitta amesema taarifa zilizosambaa juzi usiku kuwa yu
mahututi na kwamba amepelekwa hospitalini zilitolewa na wabaya wake wanochukia
msimamo wake.
Amesema yeye ni kiongozi
anayetenda haki kwa watu wote na kwamba jambo hilo lina wachukiza baadhi ya
watu wote na kwamba jambio hilo
linawachukiza baadhi ya watu ambao wanataka kupendelewa katika kila jambo.
Juzi uliibuka uvumi kuwa
sitta aliyechaguliwa kwa kishindo jana kuwa mwenyekiti wa bunge maalum la
katiba aliugua ghafla kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa bunge
hilo.
Akizungumza katika
mahojiano maalum nyumbani kwake mjini Dodoma jana sitta amesema “wabaya wangu
ndiyo waliosambaza taarifa hizo . mimi ni mzima na leo (jana) saa 2:32 asubuhi
nilirusha fomu za kugombea nafasi ya uenyekiti.
Sitta amesema
hakushangazwa na taarifa hizo kwa sababu alipoteuliwa na CCM kugombea nafasi
hiyo wapo waliopinga na kusema hawezi kugombea kwa sababu yeye ni waziri.
“Watu wengine wakadai mimi
na Andrew change aliyetaka kugombea kuwa tulikuwa tunakigawa chama niliwajibu wakati wa uchaguzi lazima watu
wagawanyike “ alisema sitta.
Katika uchaguzi wa jana
sitta alimshinda mgombea mwenzake ,
Hashimu Rungwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WABAYA WAMENIZUSHIA UGONJWA, ASEMA SITTA.”
Post a Comment