Thursday, March 13, 2014

WAMSHAURI JK KUSITISHA POSHO ZA WAJUMBE.




Vijana wa kijiji cha kitelela  katika manispaa ya Dodoma, wamemwomba Rais Jakaya Kikwete  kusitisha kwa muda malipo ya posho kwa wajumbe wa Bunge  la katiba kwa madai kuwa wako nyuma ya ratiba.

Vijana hao wamesema wajumbe hao wanaongeza muda wa  majadiliano kwa  makusudi ili siku ziongezeke  kwa ajili ya kupata posho zaidi.

 Akizungumza kwa nia ya wenzake, jumanne suswi amesema kinachofanyika katika bunge hilo ni  usanii wa kutaka serikali iwaongeze muda wajumbe ili waendelee kutafuna mamilini ya walipakodi  kwa  kigezo cha kufanya mambo kwa umakini.

Amesema kama wajumbe hao wangekuwa makini na utendaji kazi, siku 70 zingetosha kwao kufanyakazi hiyo na kutohitaji siku za nyongeza.

 Lakini kwa kuwa wameona kuwa sheria inawaruhusu kuongezwa muda, wanafanya kazi polepole na kuwap mzigo walipakodi. Amesema suswi.

 Amesema yeye na vijana wenzake kwa sasa hawana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kufuatilia mchakato huo, ili kuona jinsi  unavyoendeshwa.

 Suswi ambaye amewahi kuwa kiongozi wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) , amesema kitendo cha kutanguliza misimamo ya vyama kinamkera mno.

Bunge la kativa lilianza vikao vyake februari 18, mwaka huu na hadi sasa limechukua siku zinazofikia 25.

0 Responses to “WAMSHAURI JK KUSITISHA POSHO ZA WAJUMBE.”

Post a Comment

More to Read