Thursday, March 13, 2014

TATIZO LA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM KUWA HISTORIA.


Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.

Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.

Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.

 Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa  mitambo ya Ruvu Chini. Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Wapili Kulia).

0 Responses to “TATIZO LA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM KUWA HISTORIA.”

Post a Comment

More to Read