Thursday, March 27, 2014
MBUNGE AMTAKA MWENYEKITI SAMWELI SITTA KUMWANDIKIA BARUA RAIS KIKWETE YA KUMUOMBA ALIVUNJE BUNGE LA KATIBA.
Do you like this story?
Mbunge
Lekule Laiza amemuomba mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh. Samwel Sitta
kumwandikia barua Rais Dkt Jakaya Kikwete barua ya kulivunja bunge hilo kwa
kuwa wameshindwa kazi
Mh.
Laiza ametoa kauli hiyo leo Machi 27, bungeni wakati akichangia hoja kuhusu
upigaji wa kura ya siri ama upigaji wa kura ya wazi, na kusema kuwa wananchi
wamekuwa wakiwapigia simu na kuwataka warudi majumbani kwa kuwa wameshindwa
kazi
"Kama
kazi imetushinda na tunashindwa kufikia muafaka, ni heri mwenyekiti umwandikie
rais barua avunje bunge hili, turudi majumbani" amesema Laiza
Amesema
kuwa kutokana na bunge hilo kughubikwa na vihoja vya mara kwa mara ni dhahiri
kuwa suala hilo limekuwa likiwaumiza vichwa lakini kutokana na umuhimu wa
katiba yeye ameshindwa kuona kuwa wao kama wabunge wanafanya nini bungeni,
hivyo wanatakiwa kuondoka na kurudi kwao kwa kuwa kazi imewashinda
Kauli
hiyo imepingwa vikali na mbunge wa Arumeru mashariki Mh. Joshua Nassari
wakati akichangia hoja na kusema kuwa kwa kuwa wamekuja kwa ajili ya katiba,
anataka bunge hilo liendelee mpaka kieleweke kilichowaleta yaani kupata katiba
mpya kwa kuwa kodi za watanzania zinaendelea kutumika na hivyo inatakiwa
waendelee
"nimetoka
jimboni kwangu jana tu na ndiyo maana nimeapishwa leo, wananchi wanataka kura ya
siri na pia wanataka katiba mpya" alisema Nasari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBUNGE AMTAKA MWENYEKITI SAMWELI SITTA KUMWANDIKIA BARUA RAIS KIKWETE YA KUMUOMBA ALIVUNJE BUNGE LA KATIBA.”
Post a Comment